Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, May 29, 2010

MASHABIKI A.KUSINI WABANIWA NA BRAZIL


Brazil yawabania mashabiki Afrika Kusini

JOHANNESBURG, Afrika Kusini

TIMU ya taifa ya Brazil imewasili nchini Afrika Kusini, ikisema kuwa haitakuwa na urafiki na mashabiki na vyombo vya habari, kama ilivyofanya miaka minne iliyopita.

Habari kutoka nchini humo, zilieleza kuwa hatua hiyo ni kutokana na wachezaji na kocha kujaribu kuzuia kuzongwa na mashabiki, kitendo ambacho kinadaiwa kuliwafanya kutupwa nje ya michuano hiyo, hatua ya robo fainali nchini Ujerumani mwaka 2006.

Ilielezwa kuwa baada ya kuwasili nchini humo, timu hiyo ilikwenda kambini, ikiwa na matumaini kama walivyozoea mabingwa hao mara tano wa Dunia, lakini kwa haraka kocha Dunga akaweka wazi kuwa watajaribu kukaa mbali na mashabiki, ili kukwepa kuzingirwa na mashabiki.

“Kuanzia siku ya kwanza tulisema kipaumbele ni kwa timu ya taifa,” alisema Dunga. “Kitu kingine kitakuja baadaye kwani tunataka kufanya kazi ya timu ya taifa,” aliongeza Dunga

Naye Msemaji wa Shirikisho la Soka la Brazil, kupitia mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari nchini Afrika Kusini, alisema kilichojitokeza mwaka 2006 hakipaswi kutokea tena.

Mwaka 2006 timu hiyo ilikuwa ikifanya maandalizi yake kwenye ufukwe wa mji wa Weggis, Uswizi ambako wachezaji na kocha walisema hali ya hewa ingeifaa timu.

Wakati wa mazoezi hayo, mashabiki na waandishi wa habari walikuwa wakiruhusiwa kwenda kila mahali timu hiyo ilipokuwa ikifanya mazoezi na hatimaye, Brazil ikajikuta iking'olewa kwenye mashindano hatua ya robo fainali na Ufaransa, baada ya kuchapwa bao 1-0.

Hata hivyo mwaka huu vyombo vya habari pekee, ndivyo vitakuwa karibu na mazoezi ya timu, lakini si kwa mashabiki.

Kabla ya kuanza michuano hiyo, Brazil itacheza mechi mbili za kujipima ubavu dhidi ya Zimbabwe iyakayopigwa mjini Harare Juni 2 na mechi ya pili itakuwa dhidi ya Tanzania itakayofanyika Juni 7, mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...