Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, June 22, 2010

KERO YA JENGO LA MACHINGA COMPREX YATINGA BUNGENI


JENGO LA MACHINGA COMPREX
SERIKALI imetakiwa kutoa meelezo ya sababu za kuchelewesha kufungua soko la ‘Machinga Complex’ lililopo maeneo ya Karume Ilala Jijini Dar es Salaam ambalo lilitegemewa kufunguliwa mwaka jana ni sababu gani zimekwamisha kufunguliwa kwa jengo hilo ilianze kufanya kazi.

Hayo yamebainishwa leo bungeni mjini Dodoma wakati Mbunge wa Mgogoni kwa tiketi ya Chama CUF, Bw. Mohamed Said wakati alipokuwa akiuliza swali na kutaka kupatiwa majibu na Ofisi ya Waziri Mkuu.

Akijibu swali hilo leo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) Bi. Celina Kombani alisema kukwama kufunguliwa kwa soko la wamachinga jijini Dar es Salaam kumetokana na kuchelewa kukamilika kwa ujenzi kwani ujenzi wa soko hilo ulikuwa umekamilika na kukabidhiwa tangu Septemba mwaka 2008 na sababu ya kuchelewa kukamilika kwa ujenzi huo ni mabadiliko katika ubunifu wa mradi ambapo awali ilipangwa jengo liwe na ghorofa tatu.

Alisema kuwa wakati Mkandarasi akiwa ameanza kazi ya kuchimba msingi wadau mbalimbali walijenga hoja kwamba kuongezwe ghorofa katika jengo hilo hadi kufikia
ghorofa tano na baada ya kukubaliana kuongeza idadi ya ghorofa ili jengo liwe na uwezo wa kuchukua wanyabiashara wengi zaidi ililazimu kufanya upya usanifu wa jengo
na hivyo kuchelewa kazi ya ujenzi.

Hata hivyo alisema baada ya mkandarasi kukamilisha ujenzi wa jengo hilo tayari lilikabidhiwa rasmi kwa halmshauri ya jiji Mei 21 mwaka huu tayari kwa matumizi ambapo kwa sasa halmashauri ya jiji inakamilisha matengenezo ya vizimba na kwamba inatarajiwa hadi kufikia robo ya kwanza ya mwaka 2010/2011 jengo hilo litafunguliwa na wafanyabiashara hao wataanza kutumia jengo hilo.
JENGO LA MACHINGA

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...