Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, July 16, 2010

WIMBO WA KAFARA WAPIGWA MARUFUKU REDIONI


Pichani msanii miondoko ya Bongo Fleva,anayefahamika kwa jina la kisanii Tanzanite

Na Dina Ismail
CHAMA cha haki miliki Tanzania (COSOTA) kimezuia kupigwa kwa wimbo wa msanii chipukizi wa Bongo Fleva Mwingereza Athuman ‘Tanzanite’, ujulikanao kama ‘Kafara’, imefahamika.

Hatua hiyo inafuatia chipukizi mwingine wa bongo fleva, Nassib Abdul ‘Diamond’ kupeleka mashitaka cosota akidai kuwa Tanzanite amenakili wimbo wake wa uliompatia tunzo ya Mwanamuziki ‘Mbagala’.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, juzi Tanzania ambaye pia anajulikana kama Abuu Flava alisema kabla ya kurekodi wimbo huo aliongea na Diamond na kumuomba kufanya hivyo, alimkubalia lakini anashangaa baada ya kutoka akaenda kushitaki Cosota.

Alisema licha ya Diamond kuitwa katika vikao vya usuluhishi cosota alikuwa hatokei na mwishowe maamuzi yakatolewa, hata hivyo anasema amekubaliana na maamuzi hayo na hana kinyongo chochote.

Akienda mbali zaidi, Tanzanite alisema kilichofanya Diamond ageuke ni baada ya kuona ‘Kafara’ ni mzuri kuliko ‘Mbagala’ ndiyo maana ameingiwa na hofu, lakini hata hivyo amejipanga kikamilifu katika medani ya muziki na anatarajia kutoa nyimbo bomba zaidi.
mwisho

Na jana ndio ilikua ni siku ya kutolewa hukumu japo Diamond hakufika hata siku moja kwenye kikao cha usuluhishi...na haya yalifikiwa...

1. COSOTA watatoa matangazo kwa FM Radio zote kupiga marufuku wimbo wa KAFARA usichezwe tena!

2.Itabidi Abuu Flava amlipe fidia msanii Diamond kama akitaka.

1 comment:

  1. Pamoja na kwamba Diamond, hajasikiwa kwa upande wake, lakini sikudhani kana kuna mantiki ya COSOTA kutoa huku hiyo, mbona wanaowadhulumu watu kazi zao hawajitokezi kihivyo. Pia mwandishi wa habari hiyo kachapia, Mbagala haujampa tuzo Diamond ila Kamwambie! Kiga Boy

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...