Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, August 23, 2010

Hits Tanzania kuzinduliwa Januari 2011 kutingisha mitandao mingine


mwenyekiti wa Excellentcom Tanzania Ltd, Mhe. Abdullah Mwinyi

Mwenyekiti wa Excellentcom Tanzania Ltd, Bw.Abdullah Mwinyi (kushoto) na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo,Bw. David Charles wakipongezana baada ya kuzindua nembo ya “hits” Dar es salaam jana itakayoanza kutoa huduma za mtandao wa simu mwanzoni mwa 2011
Kampuni ya ExcellentCom inayoendesha shughuli zake kama Hits Tanzania imefanya uzinduzi wa chapa na nembo yake ya “hits”
jijini Dar es Salaam jana. Hits Tanzania ni kampuni inayoendesha mtandao wa mawasiliano ya simu ambayo imepewa leseni ya kutoa huduma za Sauti, ujumbe mfupi na huduma za Mtandao (Data).

Wakati wa uzinduzi wa nembo yake, mwenyekiti wa Excellentcom Tanzania Ltd, Mhe. Abdullah Mwinyi alisema “Hits Tanzania sasa imeanza rasmi shughuli zake na iko kwenye hatua za mwisho kuwasha mitambo yake, kwa hiyo wataanza ujenzi na upanuzi wa mtandao ili kuwa na uwezo wa kutoa huduma nchi nzima mapema mwakani".

Akizungumza na waandishi wa habari, Afisa Mtendaji Mkuu wa ExcellentCom, David Charles alisema kwamba kwa mujibu wa taarifa ya TCRA (Tanzania Communications Regulatory Authority) ya Machi 2010, soko la huduma za simu za mkononi kwa sasa zinapatikana kwa kuwafikia zaidi ya asilimia 40 ya wananchi wa Tanzania. Aliongeza kwamba na kwa mujibu wa taarifa ya BMI (British Market Index) ya awamu ya pili ya mwaka 2010, matarajio ni kwamba huduma hizo zitawafikia zaidi ya asilimia 60 ya wananchi ifikapo 2012.

Bw. Charles alisema kwamba tayari kuna uwekezaji endelevu wa miundombinu kadhaa ya mawasiliano ambayo inashawishi kuwapo kwa mikakati ya ubia endelevu. “Kusema kweli, imeonekana dhahiri kwamba hakuna wakati muafaka kwa kampuni ya Hits Tanzania kusambaza mtandao wake kama sasa,” alisema.
Kampuni itaendelea na harakati za kuwekeana mikataba na wabia muhimu ambao wataiwezesha kampuni hiyo kuwapa wateja wa Hits na wateja wa wabia huduma maalum hapo ifikapo mwakani. Kwa mtazamo huo, kampeni hiyo itaitwa "a life time subscription" ambayo itatoa thamani na ubora kwa wabia wa Hits pamoja na wateja wake.

Hits Tanzania itazindua kampeni ya kutenga namba ya simu baadae mwaka huu, ambapo wateja wataweza kutengewa namba zao kupitia kianzishi namba cha Hits, ambacho ni 0741 mpaka 8.

2 comments:

  1. what is the latest on excellentcom, its now January. Please let us know as we need to see u online soon. Anybody has last updates please let us know

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...