Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, September 18, 2010

WANAWAKE WACHUANA KATIKA POOL KUSHINDANIA NAFASI YA KUIWAKILISHA NCHI UFARANSA


Happy Ngombo Dodoma
CECILIA kILREO
zawadi na Beatrice
Beatrec Kaabuka Kagera
Zawadi Kabara Ilala

JUMLA ya timu za mikoa minane imefanikiwa kufuzu kucheza robo fainali ya mashindano ya taifa ya mchezo wa pool yanayojulikana kama 'Safari Lager National Pool Championship 2010'.
Fainali za mashindano hayo ambayo yanadhaminiwa na bia ya Safari Lager ambazo zinazofanyikia kwenye ukumbi wa Matongee Club uliopo Njiro mkoani hapa katika hatua ya awali iliyochezwa kwa mtindo wa ligi ilishirikisha mikoa 14 ya Tanzania Bara.


Timu ambazo zimefanikiwa kuingia katika hatua ya robo fainali ni mabingwa watetezi mkoa wa kimichezo wa Ilala, Kinondoni,Dodoma, Temeke, Iringa, Mbeya, Morogoro na wenyeji Arusha.Timu zilizoaga mashindano hayo ni pamoja na wageni wa mashindano hayo, Kagera na Shinyanga, Mwanza, Manyara, Tanga na Kilimanjaro.


Bingwa wa mashindano hayo anatarajia kupatikana leo kwenye kilele ambapo mgeni rasmi atakuwa Mkuu wa mkoa wa Arusha, Isdory Shirima.
Bingwa wa mashindano hayo ataondoka na fedha taslim Sh.3,500,000, huku mshindi wa pili akijizolea fedha taslim Sh.2,500,000, mshindi wa tatu Sh.1,500,000 na mshindi wa nne Sh.1,000,000.


Timu nne ambazo zitatolewa kwenye hatua ya robo fainali kila moja itaambulia kifuta jasho cha kushiriki fainali hizo cha Sh.500,000 huku timu sita ambazo hazikufanikiwa kuingia robo fainali zikiambulia Sh.250,000 kila moja.Mbali ya fainali hizo kuchezwa kwa timu kwa timu pia zinachezwa kwa mchezaji mmoja mmoja kwa wanaume na wanawake.


Na mshindi katika michezo ya wanawake atajiunga moja kwa moja na timu ya taifa ya mchezo huo kwenda kushiriki mshindano ya dunia yatakayofanyika mwezi wa kumi na moja mwaka uhu

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...