Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, December 19, 2010

PIGO JINGINE KWA WASANII ABUU SEMUHANDO 'BABA DIANA' AFARIKI DUNIA

Mkaanga chips wa siku nyingi wa Bendi ya Twanga Pepeta na bendi mbali mbali za hapa nchini,Abou Semhando a.k.a Baba Diana (pichani) amefariki dunia usiku wa kuamkia leo kwa ajali ya pikipiki .Ajali hiyo imetokea maeneo ya Tanki Bovu,Mbezi baada ya kugongwa na gari akiwa katika pikipiki yake na kutumbukia mtaroni na kupelekea mauti kumfika.Msiba upo nyumbani kwake Mwananyamala jijini Dar.
Marehemu Abou Semhando akiwa na mkongwe mwenzake Kanku Kelly katika msiba wa Dr. Remmy Ongala siku mbili zilizopita kwenye viwanja vya Biafra,Kinondoni.
Marehemu Baba Diana enzi za uhai wake akiwa na Roget Hegga,Amigolas, pamoja na MCD wakiwa nje ya club billcanas siku moja wakati bendi ya Twanga Pepeta ikipiga mahala hapo.Baba Diana atakumbukwa na wengi hasa kwa upigani wake wa drums.Mungu ailaze mahala pema peponi roho ya Marehemu Abou Semhando.

Pikipiki ya Marehemu Abou Semhando baada ya kupata ajali
Gari linalosadikiwa kuhusika na ajali hiyo likiwa mtaroni

Na John Kitime

Katika hali ya kusikitisha nalazimika kutaarifu kuwa mwanamuziki mwingine wa zamani, Abou Semhando ambaye ni mpiga drums wa miaka mingi amefariki dunia mida ya saa tisa usiku, alfajiri ya Jumamosi 18 December 2010, katika ajali ya pikipiki yake kugongwa na gari.

Marehemu Abou Semhando, maarufu kwa jina la 'Baba Diana', pia alikuwa mmoja wa waasisi na viongozi waandamizi wa The Affrican Stars 'Twanga Pepeta' kabla ya umauti kumfika. Bendi zingine alizopigia wakati wa uhai wake ni pamoja na Sola TV, Vijana Jazz na Super Matimila.


Katika ajali hiyo gari aina ya benzi imegonga nyuma pikipiki yake wakati akitoka kupiga mziki maeneo ya Africana. Alipiga drums nyimbo ya pili toka mwisho na kuelekea nyumbani ambapo ndipo alipokutana na ajali hiyo.


Jambo la kusikitisha zaidi ni kuwa Abou alikuwa mmoja ya waliokuwa wakitangulia mbele ya msafara wa mazishi ya Remmy Ongala na pikipiki y

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...