Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, April 28, 2011

BENKI YA EXIM YAAHIDI KUINUA UCHUMI WA NCHI





Na Mwandishi


WetuBenki ya Exim imeahidi kuendelea kushirikiana na serikali katika mikakatimbalimabli ya kuinua uchumi wa nchi.

Hayo yalisemwa jijini jana na Meneja Mkuu wa benki hiyo, Bwana Dinesh Arora.

Alikuwa akizungumzia ufadhili wa benki hiyo kwenye mkutano wa uwekezaji Afrikauliofanyika jijini katikati ya mwezi huu na kuhudhuriwa na maraisi watano kutokanchi zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki na wajumbe zaidi ya 900 kutoka sehemumbalimbali duniani.Alisema kuwa sekta binafsi inao wajibu mkubwa wa kuisaidia serikali kuinuauchuni na hivyo kuboresha maisha ya Watanzania.

“Exim Benki iliona fahari kubwa kufadhili mkutano huu ambao ulikuwa una lengo la kuonyesha utajiri wa rasilimali za nchi na pia kufungua fursa za kibiashara”,alisema.Bwana Arora alisema kuwa Benki ya Exim itaendelea kusaidia fursa kama hizo ilikuwawezesha Watanzania wengi zaidi kuweza kupata nafasi ya kukutana nawafanyabiashara kutoka sehemu nyingine za dunia.Alisema kuwa benki yake ina wajibu mkubwa wa kuendelea kuisaidia uchumi wan chikukua.Alisema kuwa ili wajasiriamali wa Kitanzaniia waweze kukua kibiashara na kutoamchango mkubwa zaidi kwenye uchumi,lazima ziwepo juhudi za makusudi zakuwakutanisha na wawekezaji kutoka Afrika na duniani kote. “Tunaamini kuwa maendeleo ya benki yetu yanategemea sana mafanikio ya jamiiyetu tunakofanyia kazi”alisema. Alisema pamoja na biashara benki hiyo ina jukumu la kuchangia shughulimbalimbali za kijamii na kwamba Ujasiriamali ni miongoni mwa sektazinazochangiwa kwa nguvu na benki husika.“Tumekuwa tunafanya biashara ya kibenki kama jukumu letu kuu lakini pia tumekuwana majukumu mengine kwa jamii inayotuzunguka hivyo udhamini wetu katika TEYA nimiongoni mwa utekelezaji wa majukumu hayo na kwamba Ujasiriamali tunauangaliakwa namna ya kipekee,” alisemaAliongeza kuwa katika kutambua umuhimu wa sekta ya hiyo,hivi karibuni wamefunguaakaunti mpya ya Tumaini maalumu kwa ajili ya Wajasiriamali wanawake.Alifafanua kuwa pamoja na wengine wanawake ni mhimili mkuu wa shughuli zakijamii katika familia nyingi za kitanzania hivyo benki hiyo imeona ipo haja yakipekee kuwawezesha ili nao waweze kumudu majukumu yao kwa ufanisi.Kuhusu tuzo hiyo alisema ni changamoto ya kutosha kwa Wajasiriamali nchinikatika kuhakikisha shughuli wanazozifanya zinakuwa na tija kwao binafsi na taifakwa ujumla.“Akaunti ya Tumaini ni maalumu kwa ajili ya Wajasiriamali Wanawake na hiiinaonyesha jinsi tunavyoijali sekta hii lakini pia tuzo hii ni changamoto kubwakwa wahusika kwani itawasukuma kufanya shughuli zenye tija,” alisema Bwana Arora.TEYA imelenga kutambua kazi za Wajasiriamali katika nyanja mbalimbali kutokanana mchango wao katika pato la taifa na ukuaji wa uchumi lakini pia kutoachangamoto ya ushindani kwa wahusika na sekta ya kibiashara kwa ujumla.

TEYA 2011 ilizinduliwa rasmi Machi 15 mwaka huu na inatarajiwa kutolewa baadayeNovemba ambapo Raisi Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.

Mawazo WaziriMedia Relations ManagerCapital Plus International (CPI)Phone:

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...