Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, June 19, 2011

BONANZA LA WANAFUNZI WA ZAMANI WA MAKONGO LILIVYOFANA JANA LEADERS


Wachezaji wa timu ya Netiboli ya CMTU wenye jezi nyekundu wakichuana na timu ya wanafunzi wa zamani waliowahi kusoma katika shule za Makongo na Lugalo, katika bonanza la wanafunzi waliosoma katika shule hizo lililofanyika jana, kwenye viwanja Leaders jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na wanafunzi wa sasa pamoja na walimu wa shule hizo.
Msemaji wa Bonanza hilo Mwani Nyangasa akiwapa moyo wachezaji wa timu yao ya Makongo katika bonanza hilo lililofanyika Leaders Club Konondoni.
Wachezaji wa timu ya netiboli ya CMTU wakipasiana mpira kwa madaha.
Wanafunzi wa Makongo wakipata maelezo ya huduma za benki ya NMB kutoka kwa wafanyakazi wa benki hiyo, wakati wa bonanza la wanafunzi waliowahi kusoma katika shule ya sekondari ya Makongo jana, katika viwanja vya Leaders Kinondoni jijini Dar es salaam.
Wageni waalikwa wakiwa katika bonanza hilo kutoka kulia ni Emannuel Katambo Mwalimu, Edgar Chibura Mwalimu, Kakumbi MS Mwalimu, Mayebe MH Mwalimuj, Salim Dossi Naibu Mwenyekiti Baraza la Michezo Kinondoni na Mwenyekiti wa Kwanza wa BMT, Abdul Amiri Mwalimu na WerereBugoyi Mwalimu pia.
Wanafunzi mbalimbali wa shule za Sekondari za Makongo na Lugalo wakiwa katika bonanza hilo, hapa wakishuhudia mpambano wa mchezo wa Netiboli tika ya CMTU na wanafunzi wa zamani Makongo.
http://fullshangwe.blogspot.com/

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...