Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, August 14, 2011

BFT YAWEKA HADHARANI WATAKAOWAKILISHA ALL AFRICA GAMES


SHIRIKISHO la Ngumi za Ridhaa nchini (BFT) kwa kushirikiana na kocha mkuu wa timu hiyo Raia wa Cuba Hurtado Primentel imechagua na kuwatangaza mabondia nane watakaoiwakilisha nchi katika michuano ya Mataifa ya Afrika 'All Africa Games' itakayoanza Septemba 3 mwaka huu, Maputo Msumbiji.

Mabondia hao ni Leroi John kg 52, Emilian Patrick kg 56, Nasser Mafuru kg 60, Victor Njaiki kg 64, Joseph Martine kg 69, Seleman Kidunda kg 75, Haruna Swanga kg 91 na Maximilian patrick 91+.

Akizungumza Akiwa Kibaha, Pwani Katibu MKuu wa BFT, Makore Mashaga alisema mabondia hao tayari wameanza kambi jana katika shule ya Sekondari ya Filbert Bayi iliyopo Kibaha.

"Hivi ninavyokwambia tupo njia (jana) tukielekea Kibaha, Pwani kwa ajili ya kuwapeleka mabondia wetu tayari kwa kuanza kambi yao ambayo itadumu hadi siku ya kwenda Maputo,"alisema Mashaga.

Alisema mabondia wote waliochaguliwa ni wenye uwezo mkubwa utakaoweza kuiletea sifa nchi kwenye michuano hiyo mikubwa barani Afrika na kwamba ni matarajio ya BFT mabondia hao watazingatia yale watakayoelekezwa na walimu wao.

Alisema kambi hiyo ina jumla ya watu 10 huku mabondia wakiwa nane pamoja na makocha wawili, Hurtado na kocha mzawa ambaye ni msaidizi wa Hurtado Edward Emanuel.

Mashaga alisema kambi hiyo inagharamiwa na kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) na kwamba msaada uliotolewa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) wa sh. milioni 3 utasaidia kuboresha masuala mazima ya kambi hiyo.

Ngumi ni miongoni mwa michezo sita iliyochaguliwa na Serikali kuiwakilissha nchi kwenye michuano hiyo ambapo michezo mingine ni riadha, Netiboli, Soka, PARALIMPIKI na Judo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...