Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, August 31, 2011

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AWATAKA WAISLAMU KUENDELEA KUTENDA MEMA


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati wa Swala ya Eid El-Fitr, iliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam leo Agosti 31. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, baada ya kumalizika kwa Swala ya Eid El- Fitr, iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam leo Agost, 31. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (wa pili kulia) Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi (kulia), Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Salum, wakiwa katika swala ya Eid El-Fitr, iliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo Agosti 31. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (wa pili kulia) Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi (kulia), Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Salum, wajumuika pamoja na waumini wa dini ya kiislamu kuswali swala ya Eid El-Fitr, iliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo, Agoost 31. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Na Ismail Ngayonga

Maelezo

Dar Es Salaam

MAKAMU wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal ameitaka jamii kuungana kwa pamoja katika kuhimiza maadili mema na kukemea maovu badala ya jukumu hilo kuwaachia viongozi wa dini peke yao.

Akizungumza katika sala ya Idd El Fitri iliyoswaliwa kimkoa katika viwanja vya mnazi mmoja, Dkt. Bilal alisema jamii isiwategemee viongozi wa dini katika kupambana na maovu yanayoendelea kukithiri ndani ya jamii.

Dkt. Bilal alisema kila mwanajamii kwa upande wake anatakiwa si kuacha bali pia kukataza mambo yote mabaya. “Haitoshi kwa muumini mmoja kuwa mwema peke yake, halafu akayafumbia macho maovu yanayotokea katika jamii inayomzunguka” alisema Dkt Bilal

Kwa mujibu wa Dk. Bilal alisema Watanzania hawana budi kuona fahari pia kuyatekeleza maelekezo ya mwenyezi mungu ya kuifanya dunia yote kuwa yenye neema , kwani umahiri ameutukuza mwenyezi mungu kuwa umma bora.

Dkt Bilal pia aliwashukuru waumini wa dini nyingine kwa ushirikiano wao wa dhati kwa ndugu zao waislamu, uliyoweka mazingira mazuri katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani yaliyohakikisha waumini wa kiislamu wanatekeleza ibada yao bila ya karaha na bugudha.

“Uvumilivu huo baina ya dini na uhuru uliopo wa watu kuabudu imani ya dini yao ni vitu vinavyochangia katika kuimarisha amani, umoja na upendo katika taifa letu” alisema Dkt Bilal.

Kwa upande mwingine Dkt. Bilal pia aliwataka waislamu nchini kuendelea kufanyiana mema ikiwemo kutoa sadaka, kuswali na kufanya ibada pamoja na kuwasaidia wasiojiweza mara baada ya kumalizika kwa kipindi cha mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani

Akifafanua zaidi alisema si imani safi kudhani kuwa mema yanapaswa kutendeka tu wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na badala ya hapo kuanza kufanya mambo ambayo ni kinyume na maadili.

“Napenda kuwaasa ndugu zangu waislamu kuzingatia wajibu wetu kama waumini, kufanya mambo mema na kuyaacha yote mabaya kama tunavyoamrishwa” alisema Dkt. Bilal

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...