Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, September 15, 2011

TIGO YASAIDIA SHULE YA MSINGI DAR ES SALAAM


Mtaalam wa viwango wa Tigo Pamela Shellukindo akigawa vibao kwa wanafunzi wa shule ya msingi Kawawa.
Katika jitihada zake za kusaidia sekta ya elimu nchini Tanzania, kampuni ya simu za mkononi ya Tigo imetoa msaada wa vibao vya kujifunzia 1000 kwa shule ya Msingi ya Kawawa ya jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi wa shule ya msingi Kawawa wakiwa katika picha ya pamoja.
Tigo imetoa vibao hivyo ikiwa ni katika mwendelezo wake wa kusaidia baadhi ya shule za msingi hapa nchini. Shule ambazo tayari zimekwishafaidika na msaada huo ni shule ya Msingi ya Misewe, Msisiri B, Goba na Mjimwema zote za jijini Dar es Salaam.
Shule nyingine za msingi zilizofaidika na msaada huo ni Shule ya msingi ya Uhuru na Themi za mjini Arusha.

Akiongea wakati wa kukabidhi msaada huo kwa mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya Kawawa, Mtaalam wa viwango wa Tigo Pamela Shellukindo alisema kuwa wana imani kuwa vibao hivyo vitawasaidia wanafunzi wa shule hiyo katika kujifunza mambo mbalimbali.

“Katika vibao hivi kuna michoro ya maumbo mbalimbali kama vile alfabeti, tebo ya kuzidisha na aina mbalimbali za rangi ambavyo vinaweza kumsaidia mwanafunzi,,” alisema Pamela.
Mtaalam wa viwango wa Tigo Pamela Shellukindo akimgawia ibao mwanafunzi wa shule ya msingi Kawawa kwa niaba ya wanafunzi wenzake.
Aidha Pamela alisema kuwa Kampuni ya Tigo llifikia umamuzi wa kutoa msaada huo kwa kuthamini umuhimu wa elimu ya shule ya msingi hapa nchini katika ili kuongeza nyenzo za kujifuzia mashuleni.
Mtaalam wa viwango wa Tigo Pamela Shellukindo akimkabidhi vibao Bw. Masoud Mikidadi ambaye ni mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kawawa.
Hivi karibuni kampuni ya Tigo iliendesha kampeni maalum ya Tigo Tuchange yenye lengo la kuchangia sekta ya elimu hapa nchini. Kiasi cha pesa kilichopatikana kitatumika kununua vitabu kwa jili ya kusaidia baadhi ya shule za msingi.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...