Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, November 28, 2011

MAMA ASHA BILAL MGENI RASMI KATIKA SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA MIAKA 20 YA MAENDELEO YA WANAWAKE ZANZIBAR (COWPZ)


Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akimkabidhi zawadi, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kuhamasisha Maendeleo ya Wanawake Zanzibar (COWPZ) Balozi Amina Salum Ally, kwa kutambua mchango wake katika kuendeleza na kusimamia Jumuiya hiyo, wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa Jumuiya ya Kuhamasisha Maendeleo ya Wanawake Zanzibar (COWPZ) zilizofanyika kwenye Viwanja vya Bustani ya Victoria mjini Zanzibar jana Novemba 26. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal (wa pili kulia) akikata Keki maalumu iliyoandaliwa ikiwa ni sehemu ya sherehe za maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa Jumuiya ya Kuhamasisha Maendeleo ya Wanawake Zanzibar (COWPZ) zilizofanyika kwenye Viwanja vya Bustani ya Victoria mjini Zanzibar jana Novemba 26. Wengine ni baadhi ya Viongozi wa Jumuiya hiyo kutoka (kushoto) ni Waziri wa Ustawi wa Jamii Maendeleo, Vijana Wanawakw na Watoto, Zainab Omary Juma, Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Fatma Fereji, Mke wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mama Awena Seif na (kulia) ni Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Balozi Amina Salum Ally. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Mke wa Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akijumuika na baadhi ya Kinamama waliohudhuria maadhimisho ya sherehe hizo za miaka 20 tangu kuanzishwa kwa Jumuiya ya Kuhamasisha Maendeleo ya Wanawake Zanzibar (COWPZ) zilizofanyika kwenye Viwanja vya Bustani ya Victoria mjini Zanzibar jana Novemba 26. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akizungumza na Mkuu wa Kikundi cha Nuru ya Kisauni, Hamisa Maabad Ali, wakati alipokuwa akitembelea mabanda ya maonyesho ya sherehe za maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa Jumuiya ya Kuhamasisha Maendeleo ya Wanawake Zanzibar (COWPZ) zilizofanyika kwenye Viwanja vya Bustani ya Victoria mjini Zanzibar jana Novemba 26. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akipokea maandamano ya Wanawake na Vijana, wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa Jumuiya ya Kuhamasisha Maendeleo ya Wanawake Zanzibar (COWPZ) zilizofanyika kwenye Viwanja vya Bustani ya Victoria mjini Zanzibar jana Novemba 26. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...