Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, December 28, 2011

Rais Dk. Shein ashiriki katika mazishi ya marehemu Kanali Nassor Waziri Mageta







Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk Ali Mohamed Shein,(wa tatu kulia) pamoja na Viongozi wengine wakiusalia mwili wa Marehemu Kanal Nassor Waziri Mageta,aliyekuwa Mkuu wa Kikosi cha Valantia,katika msikiti masjid Twariq Bububu nje wa mji wa Zanzibar, aliyefariki jana na kuzikwa Kijiji kwao Mkanyageni Wilaya ya Magharibi Unguja.

Wananchi wa Kijiji cha Mkanyageni Wilaya Magharibi Unguja wakilibeba jeneza la Marehemu Kanal Nassor Waziri Mageta,aliyekuwa Mkuu wa Kikosi cha Valantia,aliyefariki jana na kuzikwa Kijiji kwao Mkanyageni Wilaya ya Magharibi Unguja.

Askari wa Vikosi vya SMZ,wakilibeba Jeneza lenye mwili wa Marehemu Kanal Nassor Waziri Mageta,aliyekuwa Mkuu wa Kikosi cha Valantia,aliyezikwa jana katika kijiji cha mkanyageni Wilaya ya Magharibi mkoa wa mjini magharibi Unguja.

Askari wa Vikosi vya SMZ wakiondoa Nguo alizozitumia marehemu Kanali Nassor Waziri Mageta,aliyekuwa Mkuu wa Kikosi cha Valantia, aliyefariki jana na kuzikwa Kijiji kwao Mkanyageni Wilaya ya Magharibi Unguja.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk Ali Mohamed Shein,( katikati) pamoja na Viongozi wengine wakiwa katika maziko ya Marehemu Kanal Nassor Waziri Mageta,aliyekuwa Mkuu wa Kikosi cha Valantia, aliyefariki jana na kuzikwa Kijiji kwao Mkanyageni Wilaya ya Magharibi Unguja.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk Ali Mohamed Shein,akitia udongo katika kaburi la Marehemu Kanal Nassor Waziri Mageta,aliyekuwa Mkuu wa Kikosi cha Valantia,aliyefariki leo na kuzikwa Kijiji kwao Mkanyageni Wilaya ya Magharibi Unguja.

Askari wa Vikosi vya SMZ wakitoa salamu ya hesha katika kaburi la marehemu Kanali Nassor Waziri Mageta,aliyekuwa Mkuu wa Kikosi cha Valantia, aliyefariki jana na kuzikwa Kijiji kwao Mkanyageni Wilaya ya Magharibi Unguja. Picha na Ramadhan Othman IKULU

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...