Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, January 9, 2012

MABONDIA MANENO OSWARD NA RASHIDI MATUMLA KUPAMBANA TENA BAADA YA KUTOKA SARE


MAANDALIZI ya pambano lisilo la ubingwa kati ya mabondia Rashid Matumla ‘Snake Man’ na Maneno Oswald ‘Mtambo wa Gongo’ lililopangwa kuwa Februar 25 mwaka huu yanaenda vizuri.

Promota wa mpambano huo Issa Malanga, alisema pambano hilo limeandaliwa ili kumaliza ubishi baina ya mabondia hao, ambao pambano la mwisho walitoka sare ya point 99.99

Hata hivyo Oswald aliwalalamikia majaji kuwa hawakumtendea haki. Mabondia hao wamewahi kupambana mara nne, Oswald akishinda mara moja na Matumla mara mbili na kutoka sare mara moja.

Alisema pambano hilo linatarajia kuwa la raundi 10 uzito wa kati, litafanyika kwenye ukumbi wa PTA sabasaba Dar es salaam


Mpambano huo wa kumaliza ubishi baada ya kila mmoja wao kudai alishinda katika mpambano wao wa mwisho

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...