Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, February 22, 2012

AIRTEL YAKABIDHI MILIONI 50 KWA MSHINDI WA PILI WA MZUKA PROMO


Mshindi wa pili wa promosheni ya Airtel MZUKA Bi Khadija Omari Issa akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) huku akishuhudia kuwa tayari ammeshapata pesa hizo kwenye akaunti yake mara baada ya hafla fupi ya makabidhiano rasmi iliyofanyika katika ofisi kuu za Airtel jijini dar es salaam leo
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya kukabidhi zawadi ya shilingi milioni 50/= iliyofanyika ofisi za Airtel zilizopo Morocco kwa mshindi wa promosheni ya Airtel MZUKA wakati kulia ni Mshindi huyo Bi Khadija Omaria, wakwannza shoto ni Afisa Mawasiliano wa Airtel Bi , Dangio Kaniki leo.
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando akikabidhi hundi ya mfao ya shilingi milioni 5o/= kwa mshindi wa pili wa promosheni ya Airtel MZUKA Bi Khadija Omari Issa (kushoto) wakati Afisa Mawasiliano wa Airtel Bi Dangio Kaniki (shoto) akishudia. Makabidhiano hayo yamefanyika katika ofisi kuu za Airtel jijini dar es salaam leo.
Mshindi wa pili wa promosheni ya Airtel MZUKA Bi Khadija Omari Issa akionyesha cheki yake ya milioni 50/= zawadi alijishindia katika promosheni kabambe ya Airtel MZUKA inayoendeshwa na Airtel mara baada
ya hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika katika ofisi kuu za Airtel jijini dar es salaam leo.


Airtel yakabidhi milioni 50 kwa mshindi wa pili wa MZUKA promo
• Mshindi wa promo ya mwisho MZUKA kupatikana mwanzoni mwa Machi
• Promsheni mpya ya NANI MKALI itaendelea kufaidisha watea na zaidi ya milioni 200.

Dar es Salaam 22/02/2012 Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imekabidhi kitita cha shilingi milioni 50 kwa mshindi wake wa pili wa promosheni yao kubwa ya MZUKA inayokaribia kuisha mwishoni mwa mwezi
huu

Akiongea wakati wa makabidhiano hayo Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando alisema promosheni hii ni ya muda wa miezi mitatu na tuliahidi kutoa zawadi zenye thamani ya thamani ya hadi milioni 600/= kwa hiyo leo milioni hizi 50 zinazoenda kwa Bi Khadija Omari Issa Mkazi wa Dar es Salaam eneo la Magomeni

Kitita hicho cha Airtel MZUKA shilingi milioni 50 tayari kimewekwa katika akaunti yake na sasa anaweza kuzitumia kuanza kufanikisha mipango na malengo yake aliyojiwekea

Pia kwa kupitia Promosheni hii ya MZUKA wa Airtel tayari tumesha toa zawadi nyingine nyingi ikiwemo simu za Sumsung za kisasa zianzotumia laini mbili zaidi ya 1,200 pia Sumsung Galaxy S2 zaidi ya 360 na vile vile Sumsung Galaxy 7.0 zaidi ya 180 kwa wateja wetu mbalimbali walioko nchini Tanzania

Bado mteja wa Airtel unanafasi ya kujishindia zawadi zilizobaki kupitia promosheni ya mzuka ikiwemo zawadi kubwa ya shilingi milioni 50 ambapo itatolewa kwa mteja mmoja tarehe 2 marchi 2012. Pia bado zawadi nyingine za simu za Sumsung galaxy kila siku na kila wiki zinaendelea kutoka kama kawaida

Ili mteja aweze kushinda ni rahisi na pia ni bure. Shiriki kwa kutuma neno MZUKA kwenda 15565 na namba yako itakuwa inaingia kwenye droo bure

Nae mshindi wa pili wa promosheni Bi Khadija Omari alisema “Naishukuru sana Airtel kwa kuniwezesha kujipatia mamilioni haya ya fedha ambayo msaada mkubwa sana kwangu ninawashauri wenzangu ambao hamjashinda endeleeni kushiriki kwani mnaweza kuibuka washindi wa ili droo ya mwisho inayofuata

“Nitaitumia zawadi yangu kuboresha maisha yangu ili niweze kutimiza ndoto zangu nilizokuwa nazo tangu awali alimaliza kwa kusema Bi Khadija

Artel Tanzania inaendesha na promosheni nyingine mpya ya NANI MKALI ambapo zaidi ya milioni 200 zinashindaniwa, Ili kushiriki promosheni hiyo mteja anatakiwa kutuma nene MKALI kwenda 15656 bure na kisha ataanza kupokea maswali tofauti na kila atakapokuwa akijibu maswali hayo kwa kujibu sms hizo atapata pointi na kujiongezea nafasi ya kushinda.

Kila SMS itatozwa shilingi 350 tu hii ni pamoja na kodi. Promosheni zote za Airtel zinadhamira ya kuwazawadia wateja wote wa Airtel ambao wamekuwa wateja wazuri na kutumia huduma za Airtel kila siku.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...