Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, March 13, 2012

WASANII WA MNANDA, MDUARA, EXTRA BONGO NA IZO BUSINESS WATIKISA NDANI YA DAR LIVE

Msanii Easy Man akikamua stejini. WASANII Dogo Mfaume, Easy Man na kundi la Jaguar jana walifunika vilivyo kwa upande wa Mnanda huku Offside Trick wakisindikizwa na Hammer Q, AT na Shilole wakiangusha bonge la burudani na kuwarusha vilivyo wapenzi wa Mduara waliofurika katika ukumbi wa maraha wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem. Bendi ya muziki wa dansi ya Extra Bongo nayo haikuwa nyuma kukonga nyoyo za mashabiki wakati washiriki wa shindano la Vaa, Imba na Cheza kama Rihanna wakitikisa na kuwaacha midomo wazi wapenzi wa shangwe mahali hapo. Msanii Izo Business aliyepanda stejini kama ‘surprise’ naye alifanya kweli kwa kuwarusha mashabiki na songi lake kali la Ridhiwan.
AT na Shilole wakiwapagawisha mashabiki.
Msanii aliyepanda stejini kama 'suprise' Izo Business akiwasabahi mashabiki kwa songi lake la Ridhiwan.
Washiriki wa shindano la Vaa, Imba na Cheza kama Rihanna walioingia sita bora wakiwa katika pozi.
Nyomi iliyoitikia shangwe hizo
You might also like:

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...