Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, October 31, 2012

Serikali Kusaidia Kubana Wanaokiuka Sheria Za Filamu



Maelezo 31/10/2012 

 KAMPUNI ya usambazaji na utengenezaji filamu nchini Steps Entertainment imeahidi kushirikiana na serikali kupambana na wanaokiuka sheria ya filamu na michezo ya kuigiza ya mwaka 1976. Hayo yamesemwa jana na meneja Mkuu wa Steps Entertainment Bw. Jairaj Almoradan jijini Dar es salaam wakati wa mkutano na Sekretatieti ya Bodi ya filamu Tanzania. Bw.Almoradan amesema kampuni yake haitapokea kazi za wasanii wasiofuata sheria kwa kutengeneza filamu zilizo kinyume na maadili na zilizo kinyume na sheria. Amesema kuwa sheria inawataka kutengeneza filamu zinazofuata maadili na kuwasilisha master kopi kwa ajili ya kuidhinishwa kuingia sokoni. “tutajitahidi kuwaeleza wasanii na tutakuwa wakali kutopokea filamu ambazo tunaona zipo kinyume na maadili na utamaduni wetu.”Amesema Bw. Almoradan. Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Bodi ya Ukaguzi wa Filamu Bi. Joyce Fissoo amesema bodi imekuwa ikipata malalamiko kuhusiana na baadhi ya filamu kuwa kinyume na maadili ya Mtanzania. “Sisi kama bodi kazi yetu ni kukagua filamu na matangazo yake kama yapo kimaadili na yamefata sheria ikiwa ni pamoja na kuzipa madaraja filamu hizo kabla hazijaenda sokoni.”amesema Bi.Fissoo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...