Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, December 31, 2012

MSTAHIKI MEYA JERRY SILAA AKABIDHI ZAWADI ZA MWAKA MPYA KWA KITUO CHA TUSHIKAMANE CHILDREN CARE TRUST FUND.



Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akikabidhi Mbuzi kwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Tushikamane Children Care Trust Fund Bw. Gratho Messy Mbele (wa kwanza kulia) na Mkuu wa Shule ya Tushikamane Bi. Euphrosine Mtundu, kama zawadi kwa watoto yatima wa kituo hicho ambapo panapo majaliwa hapo kesho atajumuika nao kupata chakula cha mchana. Anayeshuhudia tukio hilo ni Diwani wa Kata ya Tabata Hajati Mtumwa Mohamedi (wa pili kushoto)

Mstahiki Meya Jerry Silaa akikabidhi ndoo ya mafuta kwa kituo hicho chenye lengo la kuhudumia watoto yatima na watoto wanaoishi katika mazingira magumu na hatarishi kwa kuwapa mahitaji muhimu kama vile elimu, afya, chakula, malazi, mahitaji ya shule, pamoja na huduma za kisaikolojia na ulinzi dhidi ya manyanyaso.

Viongozi wa kituo hicho wakimshukuru Mstahiki Meya Jerry Silaa.

Meya wa Manispaa Mstahiki Jerry Silaa akibadilishana mawazo na baadhi ya viongozi wa kituo hicho mara baada ya kukabidhi zawadi za vyakula ikiwa ni mchango wake kwa vijana hao katika kusherehekea mwaka mpya 2012/2013.
Kila mwaka wakati wa sherehe za mwaka mpya Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala yeye binafsi hutoa sadaka kwa wahitaji kwa kumshukuru Mungu kwa kumuwezesha kumaliza mwaka salama.
Leo Mstahiki Meya Jerry Silaa ametoa chakula kwa kituo cha Watoto Yatima na watoto Yatima na watoto Waishio Katika Mazingira Hatarishi cha Tushikamane Children’s Care Trust Fund ambapo pamanapo majaliwa hapo kesho atakula chakula pamoja nao.
Asasi hiyo ya Tushikamane Children’s Care Trust Fund ilianzishwa mwaka 2001 na kupata usajili wa kudumu mwaka huo huo ili iweze kujiendesha kwa mujibu wa sheria za nchi.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...