Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, December 26, 2012

WAFANYAKAZI WA BENKI YA NBC WATOA ZAWADI ZA X-MAS NA MWAKA MPYA


 Meneja Huduma kwa Wafanyakazi wa NBC, Suzyo Gwege-Nyirenda (kulia) akikabidhi msaada vyakula na vitu vingine kwa watoto wanaolelewa katika kituo cha CHAKUWAMA, Sinza jijini Dar es Salaam vilivyotolewa na wafanyakazi wa benki hiyo  ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za Sikukuu za Christmas na mwaka mpya. Wafanyakazi hao walichanga zaidi ya shs milioni 3 kwa ajili ya vitu hivyo na sehemu ya pesa itatumika kulipia ada za shule kwa baadhi ya watoto mwakani.
 Meneja Mwandamizi Idara ya Utendaji wa Benki ya NBC, Salim Rupia (kulia) akikabidhi msaada vyakula na vitu vingine vilivyotolewa na wafanyakazi wa benki hiyo kwa Katibu wa kituo cha kulelea watoto yatima cha CHAKUWAMA, Ally Saidi kituoni hapo, Sinza, Dar es Salaam juzi  ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za Sikukuu za Christmas na mwaka mpya. Wafanyakazi hao walichanga zaidi ya shs milioni 3 kwa ajili ya vitu hivyo na sehemu ya pesa itatumika kulipia ada za shule kwa baadhi ya watoto mwakani. Wengine ni baadhi ya wafanyakazi hao na watoto wa CHAKUWAMA.
Baadhi wa watoto wanaolelewa katika kituo cha CHAKUWAMA, Sinza jijini Dar es Salaam wakionyesha baadhi ya vitu walivyopewa msaada na wafanyakazi wa Benki ya NBC kituoni hapo juzi ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za Sikukuu za Christmas na mwaka mpya. Wafanyakazi hao walichanga zaidi ya shs milioni 3 kwa ajili ya vitu hivyo na sehemu ya pesa itatumika kulipia ada za shule kwa baadhi ya watoto mwakani.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...