Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, January 19, 2013

HOTPOT ZATUMIKA KUINGIZA SIMU VISU NA BANGI MAHABUSU YA SEGEREA, Kamati yabunge yaoneshwa ushahidi.


Afisa wa Magereza wa Gereza la Segerea, jijini Dar es Salaam, Gibson Mwakibibi akiwaonyesha mfuniko wa Hotpot (Chombo cha kuhifadhia chakula) pamoja na Radio Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama ambapo vifaa hivyo vinatumika kuficha simu, visu, bangi na vifaa mbalimbali ambavyo ni hatari kwa usalama wa Mahabusu na wafungwa. Vifaa hivyo vilikuwa vinaingizwa na mahabusu hao pmaoja na baadhi ya ndugu zao wanapopeleka chakula gerezani hapo. Hata hivyo, maafisa magereza kwa kutumia chombo cha kugundulia vifaa mbalimbali (Metal Detector) kinachotumika gerezani hapo huvikamata vifaa hivyo.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama, Mussa Azzan Zungu pamoja na wajumbe wa kamati yake wakiwauliza maswali mbalimbali Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza katika Gereza la Segerea lililopo jijini Dar es Salaam. Kamati hiyo ilitembelea sehemu wanapolala Wafungwa na Mahabusu, jikoni, ghala la chakula pamoja na kuzungumza na Maafisa wa Jeshi hilo na baadaye Mahabusu na Wafungwa.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Azzan Zungu akizungumza na Mahabusu na Wafungwa wa Gereza la Segerea jijini Dar es Salaam (hawapo pichani) wakati kamati yake ilipofanya ziara ya kikazi katika gereza hilo jana. Kamati hiyo ilitembelea sehemu wanapolala wafungwa na mahabusu, jikoni, ghala la chakula pamoja na kuzungumza na Maafisa wa Jeshi hilo na baadaye Mahabusu na Wafungwa.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...