Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, March 21, 2013

NMB YAZINDUA MIKOPO YA PIKIPIKI YA MIGUU MITATU




 Mkuu wa kitengo cha wajasiliamali wadogowadogo na wakati NMB filbert Mponzi (katikati)akifurahia kuzinduliwa mkopo wa pikipiki za miguu mitatu .Wateja wa NMB  wataweza kupata  pikipiki hizi za miguu mitatu kwa kupitia matawi ya NMB .Kulia ni Meneja wa Mauzo wa Kampuni ya Fair Deal Auto Ltd, Anil Dewan na Meneja Masoko wa Kampuni ya Car and General, Jonathani Masanja.
Mkuu wa Kitengo cha Wajasiriamali Wadogo Wadogo na wa Kati NMB, Filbert Mponzi (kati) Meneja  Mauzo wa kampuni ya Fair Deal Auto LTD, Anil Dewan (Kulia) na Meneja Masoko wa kampuni ya Car and General, Jonathani Masanja wakifurahia kuzinduliwa mkopo wa pikipiki za miguu mitatu kwa wateja wa NMB.

Mkuu wa Kitengo cha wajasiriamali Wadogo Wadogo na wa kati wa NMB, Filbert Mponzi (pili kulia) akimpongeza Meneja Mauzo wa kampuni ya Fair Deal Auto LTD, Anil Dewan baada ya kuzindua mkopo wa pikipiki za miguu mitatu kwa ajili ya wateja wa NMB, wakishuhudia ni Meneja Masoko wa kampuni ya Car and General, Jonathani Masanja (pili kushoto) na Meneja wa NMB tawi la Mbezi, Leonard Ngaya.


Mkuu wa Kitengo cha wajasiriamali Wadogo Wadogo na wa kati wa NMB, Filbert Mponzi (pili kulia) akimpongeza Meneja Masoko wa kampuni ya Car and General, Jonathani Masanja (pili kushoto) baada ya kuzindua mkopo wa pikipiki za miguu mitatu kwa ajili ya wateja wa NMB, wakishuhudia ni Meneja Mauzo wa kampuni ya Fair Deal Auto LTD, Anil Dewan na Meneja wa NMB tawi la Mbezi, Leonard Ngaya.


DAR ES SALAAM, Tanzania

BENKI ya NMB kwa kushirikiana na kampuni mbalimbali zinazosambaza pikipiki za miguu mitatu, imeanzisha mikopo ya pikipiki hizo kwa wateja wake kwa lengo la kuwapatia unafuu wa kujikimu kimaisha huku wakiendelea na shughuli zao za kila siku.

Mikopo hiyo yenye masharti nafuu itatolewa kwa mteja yeyote mwenye kukidhi vigezo vilivyowekwa ikiwa ni uwezo wa kulipia asilimia 30 ya gharama au bei ya pikipiki kama inavyouzwa na kampuni hizo ambazo ni Fair Deal Auto Private Ltd inayosambaza pikipiki za miguu mitatu aina ya Bajaji pamoja na kampuni ya Car and General Ltd inayosambaza inayosambaza pikipiki ya miguu mitatu aina ya TV’S King.

Akizindua huduma hiyo katika tawi la Mbezi Beach jana, Meneja Mwandamizi wa wajasiriamali wadogo na wa kati Filbert Mponzi amesema kuwa, gharama za pikipiki hizo hutofautiana kulingana na kampuni husika.

Alisema kuwa, bajaji inayosambazwa na kampuni ya Fair Deal Auto Private Ltd kwa sasa inauzwa sh. milioni 5.4 huku TV’S King inayosambazwa na kampuni ya Car and General Ltd ikiuzwa kwa sh. milioni 5.6.

Alisema, mikopo hiyo hutolewa kwa muda wa miezi 24 ambapo kwa kipindi hicho chote mteja ataendelea kurejesha makato ya kila mwezi kulingana na makubaliano yatakayofanyika baina yake na benki.

Aidha, mikopo hiyo inawekewa bima itakayomletea mkopaji unafuu wa kumalizia deni hasa pale atakapopata matatizo ya kiafya yatakayomfanya asiwe na uwezo wa kuendelea na shughuli zake za kila siku au hata kufariki kwani bima hiyo itamalizia deni na mteja ataendelea kumiliki pikipiki yake.

Aliongeza kuwa, wateja wa NMB sasa wanaweza kutimiza ndoto zao za kumiliki pikipiki ya miguu mitatu kwa kutumia mikopo hiyo.

Mikopo hiyo kwa sasa hutolewa katika matawi tisa tu ya NMB yaliyopo jijini Dar es Salaam ambazo ni NMB Temeke, NMB Tegeta, NMB Mbezi, NMB Ilala, NMB Airport, NMB Mlimani City, NMB Magomeni pamoja na NMB Msasani.

NMB haitaishia hapo kwani itaendelea kufanya mikakati mikubwa ili kuhakikisha huduma hiyo inawafikia wateja wake walioko katika mikoa mingine hapo baadaye.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...