Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, April 18, 2013

JAMII YAFAIDIKA NA MAFAO YA NSSF


Ofisa wa Matibabu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Yasinta Shibola akitoa ufafanuzi kwa watu mbambali waliotembelea banda la NSSF wakati wa maonesho ya Huduma za Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam leo ambapo NSSF ni moja ya taasisi zinazoshiriki katika maonesho hayo. 
Baadhi ya watu mbalimbali wakipata maelezo ya huduma zinazotolewa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na hasa huduma ya mafao ya matibabu iliwafutia watu wengi, wakati wa maonesho ya Huduma za Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam.
 Ofisa Uhusiano Huduma kwa Wateja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Maife Kapinga akifafanua jambo kuhusu huduma ya mafao ya matibabu wakati wa maonesho ya Huduma za Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam jana.
 Baadhi ya watu waliojitokeza katika banda la NSSF wakipata maelezo ya huduma mbalimbali za NSSF.

Na Mwandishi Wetu

WATANZANIA wametakiwa kujiunga na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), ili kufaidika na huduma za bure katika mafao yanayotolewa na shirika hilo.

Wito huo umetolewa leo na Ofisa wa matibabu wa NSSF, Yasinta Shibola, jijini Dar es salaam katika maonesho ya siku tatu ya Muhimbili kutimiza miaka 13 toka kupandishwa hadhi ya kuwa hospitali ya Taifa tangu mwaka 2000.

Shibola alisema kuwa NSSF hawatoi mafao ya kustaafu pekee bali wana mafao mengine ambayo hutolewa bure kwa mwanachama aliyejiunga na mfuko huo.

“Mafao yetu yamejikita kusaidia wateja wa sekta binafsi na wa serikali, lakini pia hata wale wanaofanya kazi kwa kujitegemea kama atakuwa mwanachama wetu atapatiwa fao hilo kama wengine tena katika hospitali atakayochagua yeye mwenyewe katika zile ambazo tumeingia nazo mkataba na kupewa fao hilo kama wengine wote, hakuna upendeleo hapo,”alisema

Naye Ofisa habari wa NSSF, Maife Kapinga, alisema kuwa fao la matibabu (SHIB) ni bure na linahudumia watu wanne katika familia moja.

Aidha alisema kuwa maonesho hayo yamekata kiu ya wafanyakazi wa Muhimbili pamoja na wagonjwa kwani wengi walikuwa hawana elimu ya namna shirika hilo linavyofanya kazi japo ni wanachama.

Kapinga alitoa wito kwa watanzania kujiunga na shirika hilo ili wafaidike na mafao yanatolewa bure.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...