Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, April 14, 2013

KING CLASS MAWE AJIPANGA KUMUHADHIBU MWAMAKULA


Kocha wa Kimataifa wa Mchezo wa Masumbwi Nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akimwelekeza bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' jinsi ya kupiga maumbwi ku kupangua ngumi za mpinzani wake
BONDIA Ibrahim  Class 'King Class Mawe' amendelea kujifua na kujiandaa 
kumkabili Amosi Mwamakula katika pambano la utangulizi wakati wa
mchezo wa kati ya Francis Cheka na Thomas Mashali.
Pambono la raundi nane linatarajiwa kufanyika katika Ukumbi wa PTA
Sabasaba, Dar es Salaam Mei Mosi  Siku ya jumatano , linatarajiwa kuwa la vuta
nikuvute kutokana na kila mmoja kujigamba kujiandaa vema.
Kocha wa King Class Mawe, Rajabu Mhamila 'Super D' alisema kuwa
bondia wake anajiandaa vema na matumaini yanaonekana baada ya kucheza Sparng na watu watano tofauti tofauto ambapo alianza kupambana na Abuu Mtambwe raundi 4,Kassimu Gamboo, nae vile vile na Ibrahimu Toll pamoja na Ally Masaga kitu ambacho kimenipa moli wa kumchakaza Mwamakula ili
kuendelea kujiwekea rekodi nzuri.
"Bondia wangu yuko katika maandalizi ya kutosha kuhakikisha anafanya
vizuri katika pambano hilo la utangulizi kati ya Cheka na  Mashali" alisema
Super D.
Kocha huyo wa kimataifa wa mchezo wa ngumi nchini, alisema kuwa
katika mchezo huo kutakuwa na CD na DVD za mafunzo wa mchezo
huo zenye mapambano makubwa ya mabondia wa ndani na nje ya nchi.
Aliongeza kuwa baadhi ya mapambano yaliyomo ni katika CD na DVD
hizo ni ya Kalama Nyilawila dhidi ya Francis Cheka, Mbwana Matumla na
Francis  Miyeyusho, Said Mundi na King Class Mawe. na Francis Cheka dhidi ya Japhet Kaseba mapambano yote mawili mbali na hivyo atakuwa akisambaza vifaa vya mchezo wa masumbwi kwa mabondia ambao awana wanaweza kumuona na kujipatia vifaa mbalimbali

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...