Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, April 14, 2013

OLE MILYA ASEMA SERIKALI HAIMUENZI SOKOINE KWA VITENDO



Na Mahmoud Ahmad, Arusha
Siku chache tu baada ya taifa kuadhimisha kumbukumbu ya kifo cha aliyekuwa waziri mkuu nchini, Edward Moringe Sokoine aliyekuwa mwenyekiti wa Uvccm mkoani Arusha, James Ole Milya ameibuka na kutamka kwamba jamii ya kimasai imetupwa  na kubaki kama yatima ndani ya nchi yao.
Millya(1)Ole Milya, alitoa kauli hiyo juzi wakati akizuru kaburi la hayati Sokoine ambapo akiongea na waandishi wa habari  alitamka kwamba serikali haimuenzi kiongozi huyo kwa vitendo na badala yake imekuwa ikipora haki za wafugaji kwa kumega ardhi yao kila kukicha.
Alisema kuwa tangu kufariki kwa Sokoine ambaye alikuwa msatari wa mbele kupigania haki za makabila yote nchini lakini kwa hali ya sasa jamii ya kimasai imetupwa na vijana wake wamebaki wazururaji na walinzi katika nchi yao.
“Jamii ya kimasai inamkumbuka Sokoine kwa masikitiko makubwa sana kwani wamebaki wazururaji na walinzi katika nchi yao”. Alisema kwa huzuni
Hata hivyo,Ole Milya ambaye kwa sasa yuko Chadema alisema kuwa marehemu Sokoine alikuwa ni kiongozi wa mfano kwa kuwa alitoa ushirikiano katika maeneo mbalimbali nchini, lakini cha ajabu serikali imeshindwa kufuata nyendo zake.
Alisema kuwa serikali imeyasahau yote mazuri aliyokuwa akiyafanya wakati wa uhai wake huku akisisitiza kuwa kwa hali ya sasa keki na taifa inaliwa na watu wachache badala ya wananchi wote.
Ole Milya alisisitiza kuwa yeye anatoka katika jamii ya wafugaji wa kimasai na isingekuwa jitihada za wafadhili wachache ambao ni wazungu kumpeleka shule leo angekuwa mlinzi katika nyumba za baadhi ya watanzania.
Hata hivyo,alisema kuwa tangu kufariki kwa Sokoine ardhi ya jamii ya kimasai imekuwa ikimegwa siku hadi siku na serikali tofauti na maeneo  mengine hapa nchini.
Alisema kuwa wachache kama yeye wataendelea kumuenzi Sokoine kwa kusema ukweli ndani ya nchi yao bila kujali vitisho vya kuuwawa au kuteswa.
“Nahaidi kuishi kama Sokoine hata kama nikitolewa vitisho vya kuuwawa niko tayari kusema ukweli bila kujali kupingwa wala kupigwa”alisema Ole Milya

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...