Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, April 18, 2013

Sumatra yaadhibu daladala 144



 Na Mwandishi Wetu
MAMLAKA ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), imekamata magari 144 ya abiria kutokana na kufanya makosa mbalimbali.
Akizungumza na wandishi wa habari  jijini Dar es Salaam leo, Ofisa Mfawidhi Kanda ya Mashariki wa Sumatra, Conrad Shiyo, alisema magari hayo yamekamatwa kuanzia mwanzoni mwa wiki hii.
Alisema kati ya magari hayo 63 yaliokamatwa ni kutokana na makosa ya kuwatoza abiria nauli kinyume na ile elekezi,  kutumia tiketi za zamani na kukatisha njia huku wakijua fika kuwa kufanya hivyo ni kosa.
“Tumegawa chati za bei kuanzia Jumatatu kwa kila gari, zenye utambuzi wa bei ya nauli za zamani na mpya hivyo kila mwananchi anayo haki ya kuoneshwa chati hiyo pindi anapotaka na akinyimwa kuiona hilo ni kosa na mhusika atachukuliwa hatua,”alisema Shio.
Aliyataja makosa mengine kuwa ni pamoja na magari 71 ambayo madereva na makondakta wake walikutwa wakiwa hawakuvaa sare za kazi na matumizi ya lugha chafu kwa abiria ambako adhabu za makosa hayo faini zake zinaanzia sh 100,000 na kuendelea.
“Nawashukuru wananchi kwa ushirikiano wao katika kufanikisha operesheni hii  ya kukamata magari haya, tunawaomba waendelee kutuletea taarifa za madereva hao ili tuweze kuwashinda wakorofi hawa wasiotaka kutii sheria za nchi”alisema Shio.
Shio alitoa wito kwa abiria kuwa wasikubali kulipa nauli na wahakikishe kuwa wanalipa nauli halali, pia ni aibu kwa abiria hao zaidi ya 31 kushindwa na watu wawili  yani kondakta na dereva wake kwa kuwaarisha wanavyotaka.
Katika hatua nyingine Sumatra imetangaza njia mpya ya Mbezi/Ubungo Maziwa na Tegeta/ Ubungo Maziwa lengo za njia hizo ni kwa ajili ya kuwasaidia abiria wanaoishia kituo cha treni ya masafa mafupi Ubungo.
Shio aliwataka wamiliki wote wanaotaka kusajili magari kwa ajili ya njia hizo zilizotajwa hapo juu wanakaribishwa.
Aliongeza kuwa barabara zitakazotumika watajulishwa wakati wa maombi ya leseni ya biashara (TLA).

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...