Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, May 30, 2013

Ashanti United haina mpango na 'Mafaza

'

Kikosi cha Ashanti kilichopanda Ligi Kuu









KLABU ya soka ya Ashanti United iliyorejea tena kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara, imeweka bayana kuwa itafanya usajili wake kwa wachezaji vijana wenye uwezo kisoka badala ya kuwakimbilia 'mafaza' wakiwa na lengo la kutaka kuendelea kuzionyesha mfano klabu nyingine umuhimu wa kuzalisha 'jeshi' lao wenyewe.
Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mbaraka Hassani aliiambia MICHARAZO kwenye mazoezi ya timu hiyo uwanja wa Msimbazi, kwamba hawatawapapatikia mafaza kwa kuhofia kuja kujichanganya mbele ya safari ilihali wamejiwekea mikakati ya kutotaka kurudi walipotoka ambapo walisota kabla ya kurudia Ligi Kuu.
Mbaraka ambaye ndiye aliyeipandisha mwaka 2004 kabla ya kuzama msimu wa 2007-2008, alisema kutoa nafasi kwa vijana kutasaidia kuwatangaza wachezaji hao kama walivyofanya miaka ya nyuma na kuwaibua mastaa kadhaa  wanaotamba hivi sasa katika soka la Tanzania.
Baadhi ya nyotga hao ni pamoja na kipa wa kutumainiwa wa Yanga, Ally Mustafa Barthez, Jabir Aziz, Juma Jabu, Mohammed Kijuso, Juma Nyosso, Deo Ngassa na wengineo.
"Hatujaanza rasmi kufanya usajili, lakini tukianza tutajikita kwa vijana zaidi kwa lengo la kuwapa nao nafasi ya kuonwa, si unajua Ashanti ni kama chuo kazi yetu kuzalisha wengine wachukue ndivyo tutakavyofanya hata safari hii kwa vile tumepania kuonyesha mfano kwa klabu nyingine," alisema Mbaraka.
Mbaraka, alisema anaamini kuwapa nafasi vijana kunasaidia kukuza soka la Tanzania kuliko kuendelea sera ya kung'ang'ania wachezajki wenye majina ambao mara nyinbgi usumbua hasa kwenye suala la masilahi ikizingatiwa klabu yao haina wafadhili zaidi ya wanachama na wadau wake kuchangishana fedha kuiendesha.
Ashanti imerejea ligi kuu msimu ujao pamoja na klabu za Rhino Rangers ya Tabora na Mbeya City na wanaendelea kupima wachezaji kwa ajili ya kupata itakaowasajili.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...