Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, May 14, 2013

CHUO KIKUU CHA ST. JOHN'S CHAFANIKIWA KUTETEA UBINGWA WAKE WA MCHEZO WA POOL


Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amosi Makalla (mwenye suti) akifurahi pamoja na wachezaji wa chuo cha St.John’s  mara baada ya kutwaa ubingwa wa ‘Safari Lager Higher Learing Pool Competition 2013’  Mkoa wa Dododma.
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amosi Makalla (katikati) akimkabidhi nahodha wa chuo kikuu cha St.John’s, Mkole Mpangala  fedha taslim Sh.500,000 mara baada ya kutwaa ubingwa wa mashindano ya ‘Safari Lager Higher Learing Pool Competition 2013’  katika mkoa wa Dodoma, (wa pili kushoto), mwenyekiti wa chama cha mchezo huo mkoani hapa (DOPA),Fred Mushi.
CHUO kikuu cha St.John's, juzi kilifanikiwa kutetea ubingwa wake wa mashidano ya mchezo wa pool kwa wanafunzi wa vyuo vikuu mkoani hapa ya 'Safari Lager Higher Learning Pool Competition 2013' baada ya kukifunga chuo kikuu cha UDOM magoli 13-3 katika mchezo wa fainali ya mashindano hayo.
Mashindano hayo  ambayo mgeni rasmi alikuwa ni Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amosi Makalla, yalifanyikia kwenye  wa Royal Village.
Jumla ya vyuo vikuu vinne vya mkoani hapa vilishiriki mashindano hayo ambayo yanadhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager.
Chuo cha St. John's kwa kutwaa ubingwa huo kwa mwaka wa pili mfululizo licha ya kujinyakuia fedha taslim Sh.500,000 pia kitauwakilisha mkoa wa Dodoma katika fainali za taifa ambazo zitafanyika kuanzia Juni mosi mwaka huu jijini Dar es salaam.
Fainali hizo zitashirikisha vyuo vinane ambavyo vitaibuka mabingwa kwenye mikoa yao ngazi ya mikoa ya mashindano hayo.
Chuo cha UDOM kwa kushika nafasi ya pili kilizawadiwa Sh.300,000 huku chuo cha CBE kilichoshika nafasi ya tatu kiliondoka na Sh.200,000 na chuo cha Mipango kilipewa Sh.100,000 baada ya kushika nafasi ya nne.
Kwa upande wa mchezaji mmoja mmoja (wanaume), Juma Daniel wa chuo cha Mipango alitwaa ubingwa huo na kujinyakulia fedha taslim Sh.150,000 na tiketi ya kushiriki fainali za taifa na Abdallah Abdallah wa chuo cha UDOM  aliyeonyesha kiwango cha hali ya juu na kujifunga kwa bahati mbaya alishika nafasi ya pilli na kupewa Sh.100,000.
Remi Jackson wa chuo cha UDOM naye alifanikiwa kutetea ubingwa wake kwa mchezaji mmoja (wanawake) na hivyo kujinyakulia Sh.100,000 na tiketi ya kushiriki fainali  za taifa za mashindano hayo na Mwanaisha Abdallah wa chuo cha CBE alipewa Sh.50,000 kwa kushika nafasi ya pili.
Kabla ya kukabidhi zawadi kwa washindi, Naibu Waziri wa Habari,VIjana, Utamaduni na Michezo, Amosi Makalla aliwapongeza wadhamini  wakuu wa mchezo huo nchini, bia ya Safari Lager kwa kuweza kuuinua mchezo huo na kuufikisha hapa ulipofika.
Makalla pia aliwapongeza viongozi wa vyama vya mchezo huo kuanzia wilaya hadi taifa kwa ushirikiano  wao ambao umeendelea kumvutia mdhamini kuendelea kuudhamini mchezo huo bila ya kurudi nyuma..
"Ni vema mkaendeleza amani na ushirikiano mlionao sasa ili mchezo wa pool uendelee kumvutia kila Mtanzania, kwa kweli ni mchezo mzuri ambao na mimi nitaanza kujifunza.
Nakwa upande wa serikali inautambua kama ilivyo michezo mingine na wizara itaendelea kuwaunga mkono katika kuuendeleza zaidi ili siku moja uweze kuiletea heshima Tanzania katika mashindano ya kimataifa,"alisema Makalla.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...