Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, May 9, 2013

MAHAKAMA KUU YAMFUTIA MASHITAKA YA UGAIDI LWAKATARE



Lwakatare
Mahakama Kuu ya Tanzania imefuta mashtaka yote ya ugaidi yaliyokuwa yanamkabili Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA Wilfed Lwakatare.

Taarifa kutoka Mahakama Kuu zinasema Mahakama Kuu imebakiza shitaka moja tu, la utekaji ambalo kimsingi ni Jinai na lina dhamana.

Taarifa zaidi zinasema ni shangwe kuu kutoka kwa wafuasi wa CHADEMA walioko mahakamani na Familia ya Lwakatare. Baadhi ya wafuasi wa CHADEMA waliohojiwa wamesema huu ni ushindi mkubwa dhidi ya udhalimu.

Mwanafamilia mmoja wa Lwakatare huku akibubujikwa machozi akasema mkono wa Mungu umeonekana dhidi ya shetani mtoa roho za watu.

Katika kesi hii Lwakatare anawakilishwa na Jopo la mawakili nguli watano ambao ni Mabere Marando,Tundu Lissu,Professor Abdallah Safari, Peter Kibatala na Naronyo Kicheere.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...