Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, December 31, 2013

TASWA FC KUPAMBA BONANZA LA TWANGA PEPETA LA MWAKA MPYA VIWANJA VYA LEADERS CLUB




Na Leca Kimaro, Dar
TIMU ya soka ya waandishi wa habari za michezo nchini, Taswa FC kesho itapambana na timu inayoundwa na wanamuziki wa bendi ya African Stars (Twanga FC) katika mechi malaum ya kukaribisha mwaka mpya.
Mechi hiyo imepangwa kwenye viwanja vya Leaders Club inatarajia kuwa na msisimko wa aina yake ambapo baada ya mechi hiyo, bendi ya African Stars itatumbuiza jukwaani kwa mujibu wa mwenyekiti wa Taswa FC, Majuto Omary.
Majuto alisema kuwa mechi hiyo itaanza saa 7.00 mchana ili kutoa nafasi kwa wanamuziki wa Twanga pepeta kupanda jukwaani kutumbuiza nyimbo zao mbali mbali ikiwa pamoja na mpya mbali mbali zitakazosikika kwa mara ya kwanza.
Alisema kuwa wameamua kucheza na Twanga Pepeta kutokana na ushindani uliopo ambapo katika mechi ya mwisho, Taswa FC ilishinda kwa mabao 3-1. Alisema kuwa ushindani wa timu hizo mbili ndiyo umepelekea kufanyika kwa mechi hiyo ambapo awali, timu ya kombaini ya Jogging itapambana na timu ya makempu ya Twanga pepeta.
Meneja wa Twanga Pepeta, Hassan Rehani alisema kuwa kiburudani wamejiandaa vizuri na wanamuziki wake wamepania vilivyo kuanza mwaka vyema ili kutoa burudani ya aina yake. “Hii ni sehemu ya zawadi ya mwaka mpya na wanamuziki wamepania kupiga nyimbo zote zilizotamba mwaka 2013 na pia watakaribisha maombi maalum ya nyimbo kutoka kwa mashabiki.
“Tuna albamu nyingi na nyimbo kibao zilizotamba, hivyo ni wakati wa mashabiki kufanya kile wanachokitaka kutoka katika bendi yetu, wamepewa fursa hiyo nasi tupo kambili kutimiza maombi yao,” alisema.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...