Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, January 10, 2014

KIKAO CHA CHANGIA TIMU YA LIPULI FC CHAFANYIKA ,WAJUMBE WATOA YA MOYONI


Wadau  wa Lipuli Fc  kutoa taasisi  mbali mbali  kutoka taasisi  za  kifedha
Mlezi  wa  timu  ya  Lipuli Fc Mkuu  wa  mkoa  wa Iringa Dr Christine Ishengoma  akifuatilia kikao  hicho
MKUU wa  mkoa  wa  Iringa  Dr Christine  Ishengoma  ameanza kutembeza  bakuri  kwa  ajili ya  kuichangia  timu  ya  Lipuli Fc inayohitaji  kiasi cha zaidi  ya  Tsh  milioni 28 ili  kufanikisha   timu  hiyo  kuendelea na  ligi  daraja  la kwanza hatua  ya pili.
Huku  akiwabana  viongozi  wa  timu  ya  Lipuli Fc  kuanza  kueleza akiba ya  fedha  ambayo wanayo hadi  hivi  sasa kabla ya  kuanza  kuchangia wadau na kuwataka  kuwa na mikakati endelevu ya  kuweka akiba ya pesa.
Wakichangia  katika  kikao  hicho wadau  wa  soka  walitaka viongozi  wa  timu ya  Lipuli Fc  kuonyesha umakini katika kuichangia   timu  hiyo kwa kueleza  mapato na matumizi  ya  fedha  na  kuwa na utaratibu  mzuri  wa  kuichangia timu  hiyo.
Katibu  wa  timu  hiyo  Wilye  Chikweo alisema  kuwa  usajili wa  timu  hiyo  utatumia  kiasi cha Tsh milioni  4  wakati kambi  ya  timu  itatumia Tsh milioni 10 pia  mipira  20  kwa  kila mpira  Tsh 50,000 pamoja na mahitaji  mengine  yakiwemo ya marekebisho ya  uwanja Tsh 200,000
Hata  hivyo  alisema  kuwa  hadi  sasa  timu  hiyo ina akaunti  namba 01J207225200 Lipuli Football club   benki  ya CRDB .
Kwa  upande  wake  mwenyekiti wa  chama  cha mpira  wa miguu mkoa  wa Iringa Eliud Mvella Wamahanji  alisema  kuwa klabu  hiyo ya  Lipuli Fc  kuwa ina tatizo kubwa .
Alisema  kuwa  ni kweli  utaratibu wa Lipuli Fc katika  kuendesha   timu  hiyo haujatumika vema .
Wamahanji  alisema  kuwa  timu  hiyo inahitaji kucheza na kusafiri  ila bado  timu  hiyo imekuwa ikiendeshwa  kiugumu ugumu kutokana na kukosa  fedha.
“pamoja na mapungufu  ambayo  timu  inayo bado  viongozi  hao wa Lipuli FC imekuwa  ikijitahidi  kuendesha   timu  hiyo na kweli  ninawaoba  sana  kuichangia  timu  ya  Lipuli Fc  ili  kuweza  kusonga  mbele  zaidi mfano CRDB wanaweza  kusema  watachangia milioni 15 na  wengine  wakachangia  milioni japo 10 kwa  kila mmoja”
Kwa  upande  wake  mlezi  wa  timu  hiyo mkuu  wa  mkoa  wa  Iringa Dr Ishengoma  alisema  kuwa hadi  sasa tayari  amefanikisha  timu  mbali mbali kusonga  mbele  katika  mikoa ambayo amepata  kufanya kazi ukiwemo mkoa  wa Ruvuma na Pwani  na kuwa  hadi  sasa bado mkoa  wa  Iringa.
Hata   hivyo  aliwataka   wadau  wa maendeleo  katika mkoa  wa  Iringa  kujitokeza  kuichangia  timu  hiyo ya  Lipuli Fc kama  sehemu ya  kufanikisha  kuutangaza  mkoa  wa Iringa kama  ulivyo mkoa  wa Mbeya na mikoa mingine ambayo imefanikiwa  kimichezo.
Pia  aliwataka  wanaotaka  kuisaidia  timu  hiyo ya  Lipuli Fc kuingiza michango  yao katika akaunti ya timu  iliyopo CRDB akaunti  namba 01J207225200 Lipuli Football club.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...