Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, February 11, 2014

KUWASILISHA MAJINA YA MABINGWA WA MIKOA MACHI 30



Vyama vya Mpira wa Miguu vya mikoa vimetakiwa kuwasilisha majina ya mabingwa wao kufikia Machi 30 mwaka huu kwa ajili ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL).
Timu zote zitakazofuzu kucheza RCL zinaruhusiwa kusajili wachezaji wapya wasiozidi watano kutoka ndani ya mkoa kwa kufanya taratibu za uhamisho. Kamati imesisitiza kuwa usajili wa RCL ni uleule uliotumika kwenye Ligi ya Mkoa.
Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyokutana Februari 6 mwaka huu imekataa ombi la Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mwanza (MZFA) kuongeza timu za Ligi ya Mkoa kutoka 20 hadi 24.
Ikiwa chini ya Mwenyekiti wake Geofrey Nyange, Kamati hiyo imesema kwa mujibu wa Kanuni ya Ligi ya Mkoa, ligi hiyo inatakiwa kuwa na timu kati ya 16 na 20, hivyo vyama vya mpira wa miguu vya mikoa vinatakiwa kuendesha ligi kwa kufuata kanuni.

Kamati hiyo imeongeza kuwa hata kama ingekubalia ombi la MZFA kiutaratibu lisingewezekana kwa vile kanuni hufanyiwa marekebisho baada ya msimu kumalizika, wakati ombi hilo limewasilishwa katikati ya msimu.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...