Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, February 24, 2014

MFUKO WA PENSHENI WA PPF WAENDESHA SEMINA KWA WAFANYAKAZI WA TANESCO WALIOHUDHURIA MKUTANO WA MAJADILIANO ULIOFANYIKA MWISHONI MWA WIKI MJINI TANGA.




Meneja wa Kanda ya Kinondoni na Tanga wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bi Zahra Kayungwa akitoa mada ya jinsi mwanachama wa mfuko wa Pensheni wa PPF anawezaje kupata mafao yake kwa haraka na kwa wakati pindi anapostaafu kazini katika mkutano uliofanyika kati ya Wafanyakazi wa Tanesco na Maofisa wa mfuko wa Pensheni wa PPF uliofanyika mwishoni mwa Wiki mjini Tanga.
Afisa Mwandamizi wa Uwekazaji Kutoka Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bw Godbless Robin akielezea jinsi PPF inavyowekeza katika Kujenga Nyumba za Bei nafuu na kuwauzia pamoja na Kuwakopesha wanachama wao waliojiunga na Mfuko wa Pensheni wa PPF kwenye mkutano na wafanyakazi wa Tanesco uliofanyika katika Hoteli ya Navera iliyopo mjini Tanga.
Meneja wa kanda ya Kinondoni na Tanga wa mfuko wa Pensheni wa PPF, Bi Zahra Kayungwa akiwaelezea baadhi ya wafanyakazi wa Tanesco juu ya faida wanazopata wanachama wa PPF mara baada ya kujiunga katika Mfuko huo,katika Mkutano uliofanyika jijini Tanga Mwishoni  mwa wiki katika hoteli ya Navera.
Katibu Mkuu Msaidizi wa Tuico Makao Makuu, Bw Perese Jonathan akichangia mada wakati wa mkutano wa Tuico Kati ya Wafanyakazi wa Tanesco na Maafisa wa Mfuko wa Pensheni wa PPF kwenye mkutano uliofanyika mjini Tanga Mwishoni mwa Wiki.
Meneja wa Kanda ya Kinondoni na Tanga wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bi Zahra Kayungwa akiwafundisha wafanyakazi wa Tanesco kanuni ya jinsi ya kupata mafao ya Mkupuo na mafao ya kawaida ya Kila Mwezi kutoka mfuko wa Pensheni wa PPF katika mkutano uliofanyika Mjini Tanga mwishoni mwa Wiki, Anayeshuhudia kushoto ni Afisa wa PPF, Bi Chevu Sepeku.
Meneja Mahusiano na Masoko wa mfuko wa Pensheni wa PPF,  Bi Lulu Mengele akisisitiza jambo wakati akichangia mada kwenye mkutano wa Tuico Tanesco uliofanyika Katika Hoteli ya Navera Mjini Tanga Mwishoni Mwa Wiki.
Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa majadiliano wa TUICO tawi la Tanesco ambao pia ni wafanyakazi wa Tanesco wakinyanyua mikono juu tayari kwa kuuliza maswali kwa maofisa wa mfuko wa pensheni wa PPF ambao ndio walikuwa waendesha mada katika mkutano huo uliofanyika mwishoni mwa wiki Mjini Tanga katika Hoteli ya Navera.
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa majadiliano wa Tuico tawi la Tanesco wakipitia vitabu vya PPF kwaajili ya kujiongezea uelewa kuhusu mfuko wa Pensheni wa PPF kwenye mkutano wa majadiliano wa Tuico tawi la Tanesco uliofanyika mwishoni mwa wiki mjini Tanga.
Mwenyekiti wa TUICO Tanesco Tawi la Mwanza, Bw. Salehe Mkele ambae pia ni Msimamizi wa Wasoma Mita Tanesco Mwanza, akitoa ushuhuda wake wa jinsi ya baadhi ya wafanyakazi wa Tanesco Mwanza ambao wamekopeshwa na walionunua nyumba za Bei Nafuu zilizokuwa Zikiuzwa na Mfuko wa Pensheni wa PPF.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...