Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, February 12, 2014

UMOJA WA MATAIFA WASISITIZA UMUHIMU WA KUWA NA UTAMADUNI MZURI WA KUENZI WANAWAKE WANAOLETA MABADILIKO KWENYE JAMII


DSC_0017
Picha juu na chini ni Mwandishi wa habari na mpiga picha kutoka Ufaransa, Pierre-Yves Ginet akizungumza na wanafunzi wa shule za sekondari mbalimbali za jijini Dar es Salaam na kuwaonyesha picha na kuwapa ufafanuzi wa mambo mbalimbali ambayo wakinamama wamekuwa wakifanya kwa mustakabali kwa kuleta usawa na haki za wanawake duniani.

Shirika la Ufaransa la Alliance Francaise de Dar es Salaam liliandaa safari ya maonyesho iliyopewa jina “women in Resistance by the talented French photo-journalist Pierre-Yves Ginet.

Mwandishi wa habari huyo mpiga picha Pierre-Yves Ginet ambaye alifanya kazi ya kutafuta wanawake wanaojituma katika maisha yao ya kila siku na kazi zake zimeweza kuwapa ari na moyo wakinamama wengi Afrika.

Kati ya 2001 na 2006, alisafiri zaidi ya nchi 17 akipiga picha za wakinamama ambayo katika shughuli zao waliweza kufungua ukurasa mpya na kubadilisha historia katika kizazi cha leo.

Katika shughuli na katika njia tofauti walizotumia katika kubadilisha maisha wa wakinamama wengi duniani, wanawake kupitia kazi za picha Ginet wameweza kuwa na dhamira moja kubwa nayo ni kubadilisha maisha ili kuweza kuwa matumaini ya kuwa na maisha bora zaidi kwa sasa na baadaye.

Maonyesho hayo ya lengo la kuwapa usawa wakinamama wote kupitia mabara yote hapa duniani na hasa nchi zinazoendelea, sehemu za vita.

Na sehemu kubwa ya picha hizo zinaonyesha jinsi wakinamama wanavyopambana ili kujikwamua katika unyonge na ukandamizaji wa aina yoyote hapa duniani. KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...