Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, February 20, 2014

WATAALAMU CHUO KIKUU WATOA RIPOTI YA UZIMAJI WA MITAMBO YA ANALOJIA


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
UZIMAJI MITAMBO YA MFUMO WA UTANGAZAJI WA ANALOJIA AWAMU YA PILI
1.0  UTANGULIZI
Mamlakaya Mawasiliano imepokea matokeo ya tathmini ya zoezi la uhamaji toka mfumo wa utangazaji wa analojia kwenda kidijitAali.

 Zoezi hili lilifanyika kwenye miji saba kama ilivyotajwa kwenye taarifa iliyotolewa na wataalamu wa Chuo kikuu cha Dar e salaam waliofanya tathmini ya Uzimaji wa Mitambo ya Analojia katika Awamu ya Kwanza.

Mamlakaya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilifanya kamisheni kwa Chuo Kikuu cha Dar es salaam kufanya tathmini ya uzimaji wa Mitambo ya Analojia katika Awamu ya Kwanza, ikitambua kuwa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam kuna wataalamu wenye uzoefu mkubwa wa kufanya tathmini za aina mbalimbali, na kwamba uzoefu huo utasaidia sana kuhakikisha kuwa tunapata taarifa ya uhakika itakayotuwezesha kuboresha zoezi hili kwenye awamu inayofuata.

Nachukua nafasi hii kuwapongeza wataalamu waliohusika katika tathmini hii kwa weledi wao kwenye kazi hii muhimu kwa taifa letu kulingana na matokeo yaliyowasilishwa kitaalamu mbele yenu waandishi wahabari leo hii.
Tanzania ninchiya kwanza kuzima mitambo ya analojia Barani Afrika. Uamuzi wa kufanya hivyo, na matokeo yake, umeiletea sifa kubwa nchi yetu kwa jinsi ambavyo Tanzania ilijipanga na kutekeleza maazimio yaliyofikiwa kimataifa kwa wakati na weledi mkubwa. 

Hii imeonyesha wazi jinsi Serikali ilivyo weza kushirikiana na taasisi zake pamoja na wadau wote katika kutimiza azma hii iliyoafikiwa kimataifa tangu 2006.
Zoezi la uzimaji mitambo kwa awamu ya kwanza iliyoanza taree 31 disemba 2013 haikuwa rahisi kama wengi wetu tunavyoweza kufikiria, kwani liligusa nyanja nyingi zikiwemo za kijamii, kibiashara, kiufundi na Kisiasa. 

Mamlaka kama mdhibiti wa sekta ya Mawasiliano, ilibidi kuzingatia matakwa ya nyanja zote na wadau mbalimbali bila kuathiri utoaji wa habari nchini. 

Inakadiriwa kuwa mpaka kumaliza zoezi hili, mitambo ya kurushia matangazo kwa mfumo wa analojia isiyopungua 60 itakuwa  imezimwa. 

Hali hii imefanya Tanzania kuwa nchi ya pekee na kuifanya nchi yetu kuwa kituo cha mafunzo kwa nchi nyingi ambazo sasa zimeku wazi kufika kujifunza hapa nchini.
Uamuzi wa kufanya mkutano wa nchiza SADC na ule wa nchi za Jumuiya ya Madola kuhusu Mfumo mpya wa utangazaji wa kidijitali kwa sekta ya utangazaji hapa nchini hivi karibuni, matokeo ya mafanikio makubwa tuliyoyapata kwenye zoezi hili lililoendeshwa kitaalamu na Serekali yetu kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).
1.0          UPELEKAJI WA MKONGO WA TAIFA KWENYE VITUO VYA KURUSHIA MATANGAZO.
Mamlaka ya Mawasiliano kwa kushirikiana na Wizara na Kampuni ya Simu ya TTCL tuko kwenye mchakato wa kuhakikisha kuwa vituo vyote vya kurushia matangazo vinafikiwa na mkongo waTaifa (Optic fiber cable).

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...