Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, March 14, 2014

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AHITIMISHA SHEREHE ZA MIAKA 10 YA SIKU YA PAI TANZANIA.


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea Maandamano ya Wanafunzi na Walimu wa Shule za Sekondari, Msingi na Vyuo Vikuu, wakati wa Sherehe za maadhimisho ya miaka 10 ya Siku ya Pai Tanzania, iliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo.
 Sehemu ya Wanafunzi na Waalimu, wakipita mbele ya mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakiwa na mabango yenye ujumbe kuhusiana na Sherehe za maadhimisho ya Siku ya Pai Tanzania, zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo.
 Sehemu ya Wanafunzi na Waalimu, wakipita mbele ya mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakiwa na mabango yenye ujumbe kuhusiana na Sherehe za maadhimisho ya Siku ya Pai Tanzania, zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo.
 Wanafunzi wa Shule ya Msingi Uhuru Wasichana wakitoa burudani ya kwaya wakati wa sherehe hizo Mnazi Mmoja leo.
 Wanafunzi wa Shule ya Msingi Umoja ya Kiwalani, jijini Dar es Salaam, wakitoa burudani ya ngoma w Makhirikhiri, wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya Pai Tanzania, zilizofanyika kwenye viwanja vya  Mnazi Mmoja leo.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi, Julian Ilunga, wa Shule ya Sekondari Kitangili Mwanza,  aliyeibuka mshindi wa kwanza katika shindano la ‘Junior Mathematics Contest 2013’ wakati wa sherehe za maadhimisho ya Siku ya Pai Tanzania, zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadiHaji Hassan, wa Shule ya Sekondari Feza Boys ya Jijini Dar es Salaam,  aliyeibuka mshindi wa pili  katika shindano la ‘Junior Mathematics Contest 2013’ wakati wa sherehe za maadhimisho ya Siku ya Pai Tanzania, zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi, Pelucy John, wa Shule ya Sekondari Nganza Mwanza,  aliyeibuka mshindi wa kwanza kwa wasichana katika shindano la ‘Senior  Mathematics Contest 2013’ wakati wa sherehe za maadhimisho ya Siku ya Pai Tanzania, zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia moja ya vitabu wakati alipokuwa akitembelea katika mabanda ya maonyesho kwenye sherehe za maadhimisho ya siku ya Pai Tanzania, leo kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia moja ya vitabu wakati alipokuwa akitembelea katika mabanda ya maonyesho kwenye sherehe za maadhimisho ya siku ya Pai Tanzania, leo kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya uchapishaji Vitabu ya GDY Publications Co. Ltd, Gabriel Kitua. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na kuagana na baadhi ya wanafunzi , wakati akiondoka kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, baada ya kuhitimisha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Pai Tanzania. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na wanafunzi waliofanya vizuri katika shindano la ‘Senior & Junior  Mathematics Contest 2013’, baada ya kuwakabidhi zawadi zao, wkati wa sherehe za maadhimisho ya Siku ya Pai Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...