Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, March 18, 2014

MSAMA AIPONGEZA BASATA KWA KUANZISHA MAFUNZO YA SANAA KWA WATOTO


 Baadhi ya watoto wa Shule za Msingi kutoka Wilaya ya Ilala wakionesha vipaji vya kucheza ngoma wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya sanaa yaliyoandaliwa na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata),na kufadhiliwa na Kampuni ya Msama Promotions . Jumla ya watoto 200 wamenufaika na mafunzo hayo.
  Mmoja wa wanafunzi akionesha mitindo ya mavazi.
 Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Buguruni Visiwi wakionesha mitindo mbalimbali wakati wa hafla hiyo.
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akizungumza katika hafla ya kufunga mafunzo ya sanaa kwa watoto yaliyofanyika jijini Dar es Salaam. Mafunzo hayo yaliandaliwa na Basata na kudhaminiwa na Kampuni ya Msama Promotions. Kushoto ni Kaimu Katibu Mtendaji wa Basata, Godfrey Mngereza na Ofisa Tawala wa Kampuni ya Msama Promotions, Hamis Mussa.
Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), Godfrey Mngereza akizungumza wakati wa hafla hiyo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...