Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, May 16, 2014

Wanaharakati Waandamana Kupinga Utekaji wa Wasichana Nigeria


Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao, Bi. Lilian Liundi (aliyeshika kipaza sauti) akisoma barua maalumu iliyotumwa kwa ubalozi wa Nigeria nchini Tanzania kuonesha wanaharakati hao kupinga utekaji wa wasichana uliofanyika Nigeria. Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao, Bi. Lilian Liundi (aliyeshika kipaza sauti) akisoma barua maalumu iliyotumwa kwa ubalozi wa Nigeria nchini Tanzania kuonesha wanaharakati hao kupinga utekaji wa wasichana uliofanyika Nigeria.Mkurugenzi wa WiLDAF, Dk. Judith Odunga, akizungumza kupinga ukatili uliofanywa kwa wanafunzi wa kike kutekwa na kitendo cha Jeshi la Polisi nchini Tanzania kuzuia maandamano hayo ya wanaharakati.  
Mkurugenzi wa WiLDAF, Dk. Judith Odunga, akizungumza kupinga ukatili uliofanywa kwa wanafunzi wa kike kutekwa na kitendo cha Jeshi la Polisi nchini Tanzania kuzuia maandamano hayo ya wanaharakati.Viongozi wakuu wa Mtandao wa Mashirika Huru ya Kijamii (CSOs) wakipokea mabango yenye jumbe anuai za kupinga vitendo vya kikatili vilivyofanywa  na wanamgambo wa Boko Haram. Viongozi wakuu wa Mtandao wa Mashirika Huru ya Kijamii (CSOs) wakipokea mabango yenye jumbe anuai za kupinga vitendo vya kikatili vilivyofanywa na wanamgambo wa Boko HaramBaadhi ya wanafunzi wa kike na wanaharakati wakiandamana kupinga vitendo vya kikatili vinavyofanywa na kundi la wanamgambo wa Boko Haram. Baadhi ya wanafunzi wa kike na wanaharakati wakiandamana kupinga vitendo vya kikatili vinavyofanywa na kundi la wanamgambo wa Boko Haram.Baadhi ya wanaharakati na wanahabari wakisikiliza sauti za viongozi wakuu wa Mtandao wa Mashirika Huru ya Kijamii (CSOs) mara baada ya kupokea maandamano ya wanaharakati na wanafunzi kupinga utekaji wa wanafunzi wasichana uliofanyika na kikundi cha wanamgambo wa Boko Haram. Baadhi ya wanaharakati na wanahabari wakisikiliza sauti za viongozi wakuu wa Mtandao wa Mashirika Huru ya Kijamii (CSOs) mara baada ya kupokea maandamano ya wanaharakati na wanafunzi kupinga utekaji wa wanafunzi wasichana uliofanyika na kikundi cha wanamgambo wa Boko Haram.Baadhi ya wanafunzi wakiwa na huzuni kwenye maandamano hayo. Baadhi ya wanafunzi wakiwa na huzuni kwenye maandamano hayo.Baadhi ya wanaharakati na wanahabari wakisikiliza sauti za viongozi wakuu wa Mtandao wa Mashirika Huru ya Kijamii (CSOs) mara baada ya kupokea maandamano ya wanaharakati na wanafunzi kupinga utekaji wa wanafunzi wasichana uliofanyika na kikundi cha wanamgambo wa Boko Haram. Baadhi ya wanaharakati na wanahabari wakisikiliza sauti za viongozi wakuu wa Mtandao wa Mashirika Huru ya Kijamii (CSOs) mara baada ya kupokea maandamano ya wanaharakati na wanafunzi kupinga utekaji wa wanafunzi wasichana uliofanyika na kikundi cha wanamgambo wa Boko Haram.Mkurugenzi wa WLAC, Theodosia Muhulo (aliyeshika kipaza sauti) akizungumza katika mkutano na  wanahabari mara baada ya maandamano ya Mtandao wa Mashirika Huru ya Kijamii (CSOs) na wanaharakati wengine kupinga utekaji wa wanafunzi wasichana uliofanyika na kikundi cha wanamgambo wa Boko Haram. Mkurugenzi wa WLAC, Theodosia Muhulo (aliyeshika kipaza sauti) akizungumza katika mkutano na
wanahabari mara baada ya maandamano ya Mtandao wa Mashirika Huru ya Kijamii (CSOs) na wanaharakati wengine kupinga utekaji wa wanafunzi wasichana uliofanyika na kikundi cha wanamgambo wa Boko Haram.

MTANDAO Mtandao wa Mashirika Huru ya Kijamii (CSOs) nchini Tanzania pamoja na baadhi ya wanafunzi wa kike shule kadhaa za Sekondari jijini Dar es Salaam umefanya maandamano kupinga kitendo cha kikatili kilichofanywa na kikundi cha Boko Haram cha nchini Nigeri cha kuwateka wanafunzi wa kike na kuwashikilia.

Maandamano hayo ya ndani yaliyoshirikisha wanaharakati mbalimbali yamefanyika ndani ya viwanja vya TGNP Mtandao eneo la Mabibo jijini Dar es Salaam, ambapo viongozi wa mashirika yanayounda CSOs walipokea maandamano na kusoma barua maalumu yenye ujumbe wa kupinga utekaji uliofanyika na kuishinikiza Serikali ya Nigeria itekeleze matakwa ya watekaji ili wanafunzi waliotekwa waachiwe huru.

Akisoma barua hiyo kwa niaba ya CSOs, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao, Bi. Lilian Liundi alisema mashirika yao yanaotetea haki za wanawake na watoto yameamua kuungana na mitandao na wanaharakati wengine duniani kote kulaani kitendo cha kinyama cha kuwateka nyara wasichana wanafunzi zaidi ya 200 waliokuwa shuleni nchini Nigeria, tukio lililofanywa na wanamgambo wa kikundi cha Boko Haram.

"...Kwa pamoja tunakitaka kikundi cha Boko Haram kuwaachia mara moja watoto hao na kuwarudisha haraka majumbani kwao! Kama wanaharakati na watetezi wa haki za wanawake na wasichana tunaitaka serikali ya Nigeria kuchukua hatua zote muhimu zinazotakiwa ili kuokoa maisha ya wasichana hao wasio na hatia, na
kuwahakikishia haki yao ya msingi ya kupata elimu na kutembea kwa uhuru bila vitisho," alisema Bi. Liundi.

Alisema mashirika hayo yametumia maadhimisho ya siku ya kimataifa ya familia ulimwenguni kulaani kitendo hicho cha kikatili na kuitaka Serikali ya Nigeria kuhakikisha inawajibikaji ipasavyo ili kuwarejesha mateka hao mara moja tena wakiwa salama.

"Tunaikumbusha serikali ya Nigeria kuzingatia na kutekeleza tamko la Umoja wa Mataifa la haki za watoto (United Nations Convention on the Rights of the Child (CRC) ambalo liliridhiwa na Tanzania mwaka 1989 na Nigeria mwaka 2003. Mwisho tunatoa wito kwa viongozi wote wa Afrika na jumuia ya kimataifa kuimarisha ulinzi wa wanawake na watoto ili kuhakikisha tukio kama hili halitokei tena mahali pengine," alisema Liundi akisoma barua maalumu itakayowasilishwa ubalozi wa Nigeria.

CSOs wamelazimika kufanya maandamano hayo ya ndani baada yale ya kutaka kuandamana hadi Ubalozi wa Nigeria kuzuiwa na Jeshi la Polisi kwa sababu kadhaa. Hata hivyo baadhi ya askari polisi walikuwa pembeni mwa viwanja vya TGNP Mtandao katika huku zoezi la maandamano ya ndani likiendelea. Baadhi ya Mashirika yanayounda CSOs ni pamoja na TAMWA, TGNP Mtandao, WiLDAF, LHRC.

*Imeandaliwa na www.thehabari.com

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...