Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, September 29, 2014

Mke wa Waziri Mkuu achangisha Milioni 128 kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa jijini Dar


Mke wa Waziri Mkuu,MamaTunu Pinda akipokea kiasi cha dola elfu moja kutoka kwa Mkurugenzi wa Masoko utafiti na huduma kwa wateja wa Benki ya CRDB,Tully Esther Mwampamba kama mchango wake wa kuendeleza ujenzi wa Kanisa la kiinjili Moroviani Tanzania (KKMT) Mburahati jijini Dar es salaam.kulia ni Askofu David Martin Mwalyambile wa kanisa hilo Mama Pinda alikuwa mgeni rasimi katika kuendesha harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa hilo ambapo kuliweza kupatikana kiasi cha shilingi milioni mia moja na ishirini na nane.Picha na Chris Mfinanga
Mke wa Waziri Mkuu,Mama Tunu Pinda akimshukuru mtoto Cecylia Mashaka Mwaisaka mwenye umri wa miaka mitatu kwakuchangia shilingi elfu ishirini kama mchango wake wa kuendeleza ujenzi wa Kanisa la Moroviani mburahati jijini Dar es salaam.Mama Pinda alikuwa mgeni rasimi katika kuendesha harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa hilo ambapo kuliweza kupatikana kiasi cha shilingi milioni mia moja na ishirini na nane.
Kwaya ya kanisa la Moroviani Mburahati ikitumbuiza katika sherehe ya kuchangia ujenzi wa Kanisa lao.
Picha ya pamoja.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...