Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, November 7, 2014

MABONDIA SAMSON MAISHA NA IBRAHIMU TAMBA WATAMBIANA KUZIDUNDA JUMAPILI NOVEMBA 9 MANYARA PARK MANZESE

Bondia Maisha Samson kushoto wakitunishiana misuli na Ibrahimu Tamba wakati wa utambulisho wa mpambano wao utakaofanyika jumapili ya novemba 9 katika ukumbi wa manyara park tandale CCM Picha na SUPER D BLOG
Bondia Maisha Samson kushoto wakitunisha misuli na Ibrahimu Tamba wakati wa utambulisho wa mpambano wao utakaofanyika jumapili ya novemba 9 katika ukumbi wa manyara park tandale CCM Picha na SUPER D BLOG
Samson Maisha
Ibrahimu Tamba
Mabondia Ibrahimu Tamba wa Dar kushoto  na Samson Maisha wa Kyela Mbeya wakinyoshwa mikono juu na mratibu wa mpambano huo Jafari Ndame wakati wa utambulisho wa mpambano wao utakaofanyika Jumapili ya Novemba 9 katika ukumbi wa Manyara Park Tandale CCM  Picha na SUPER D BLOG
Mabondia Ibrahimu Tamba wa Dar na Samson Maisha wa Kyela Mbeya wakitunishiana misuli wakati wa utambulisho wa mpambano wao utakaofanyika Jumapili ya Novemba 9 katika ukumbi wa Manyara Park Tandale CCM katikati ni mratibu wa mpambano huo Jafari Ndame Picha na SUPER D BLOG


NGUMI KUPIGWA JUMAPILI MANZESE UKUMBA WA MANYARA

Na Mwandishi Wetu
BONDIA Samsoni Maisha wa kyela Mbeya amewasili jijini Dar es salaam na kutamba kunyakuwa ubingwa wa TPBO kwa kumpiga Ibrahimu Tamba  wakati wa mpambano utakaofanyika novemba 9 mwaka huu katika ukumbi wa Manyara Park Manzese Dar es salaam

mpambano huo wa raundi kumi kugombania ubingwa wa taifa  unaotambuliwa na TPBO utatanguliwa na mpambano mwingine wa ubingwa kati ya julius Kisarawe na

Moro Best mpambano wa raundi kumi pia mwandaaji wa mpambano huo Jafari Ndame amesema maandalizi yote yapo tayali hivyo wanasubili siku tu kukamilisha mpango mzima

aliongeza kuwa siku hiyo kutakuwa na mapambano mengine ya utangulizi ambapo Karim Ramadhani atapambana na Stevin Kobelo na Robinson Msimbe atamenyana na Fadhili Boika na mipambano mingene mikali zaidi siku hiyo kutakuwa na michezo ya utangulizi zaidi ya nane yenye raundi sita sita

katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na ulinzi wa kutosha kabisa kutokana na kujipanga vizuri katika swala hilo  kingilio ni shilingi, 5000; kwa kila mtu mchezo huu utapambwa na burudani mbalimbali

siku hiyo pia kutakuwa zikiuzwa DVD mpya za masumbwi ambazo zinaonesha mafunzo mbalimbali ya mchezo wa ngumi yanavyoanza hatua kwa hatua

mpaka kujua kitu kamili katika

mchezo huo pia kunakuwa na mapambano ya mabondia mabigwa wa dunia wa mchezo huo kama Floyd


Maywether, Manny Paquaio,mike Tyson, Mohamed Alli pamoja na mabambano ya ngumi ya ndani

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...