Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, February 16, 2015

OMARI KIMWERI AMPIGA TAFU VIFAA KOCHA KINYOGOLI

Mwanasoka wa kike, Melanie Gines ambaye ni raia wa Hispania. kushoto akimkabidhi glove kocha mkongwe wa mchezo wa masumbwi nchini zilizotolewa nabondia Mtanzania anayefanya kazi zake nchini Deer Park, Victoria, Australia, Omari Kimweri katikati kwa kushirikiana na kocha Rajabu Mhamila 'Super D' Picha na SUPER D BOXING NEWS
Bondia Om ari Kimweri akimvisha mkanda wa ubingwa wa taifa Alphonce Mchumiatumbo baada ya kumtwanga Iddi Bonge kwa point Picha na SUPER D BOXING NEWS
Bondia Mtanzania anayefanya kazi zake nchini Deer Park, Victoria, Australia, Omari Kimweri kushoto akiwa katika picha ya pamoja na kocha Habibu Kinyogoli kulia ni Mwanasoka wa kike, Melanie Gines ambaye ni raia wa Hispania

Omari Kimweri akiwa na alphonce mchumiatumbo baada ya kumvalisha mkanda wa ubingwa wa taifa
Na Mwandishi Wetu



BONDIA Mtanzania anayefanya kazi zake nchini Deer Park, Victoria, Australia, Omari Kimweri mwishoni mwa wiki iliyopita kwa mara ya kwanza ali ongea na wapenzi wa mchezo wa masumbwi ambao walifulika katika ukumbi wa P.T.A sabasaba jijini Dar es salaam

na kukabidhi vifaa vya mchezo wa masumbwi kwa kocha Habibu Kinyogoli kwa ajili ya kuendeleza mchezo wa masumbwi nchini baada ya kupokea msaada huo Kinyogoli alisema kuwa haya ni matunda yake japokuwa ni watu wachaxhe sana wanaokwenda nje ya nchi kuwakumbuka wenzao yeyey amewakumbuka wenzake kwa kuwa vifaa hivyo vitatumika na mabondia chipkizi

makabidhiano hayo yalifanyika wakati wa mpambano wa Aliphonce Mchumiatumbo na Iddi Bonge mpambano ambaso ulisha kwa K,O ya raundi ya kwanza baada ya bondia Bonge kupigwa ngumi kali na kwenda chini mara tatu kwa kila ngumi aliyokuwa akipigwa

baada ya ushindi huo Kimweri alimvalisha mkanda wa ubingwa wa taifa unaotambulika na chama cjha ngumi za kulipwa nchini P.S.T

kwa Mchumiatumbo baada ya kumgalagaza Bonge bila ya huruma katika mapambano mengine ya utangulizi bondia machachali Vicent Mbilinyi alimgalagaza bondia Khalidi Manjee bila ya huruma wakati Mussa Sunga alimchapa Makali Mawe kwa point

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...