Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, October 13, 2015

Pichaz za utoaji wa Tuzo za TASWA 2015 na Rais Jakaya Kikwete akipewa Tuzo ya heshima


Hatimaye lile tukio la utolewaji wa Tuzo za chama cha waandishi wa habari za michezoTanzania (TASWA) ambazo hutolewa kila mwaka kwa wanamichezo wanaofanya vizuri, zimekamilika usiku wa October 12 kwa wanamichezo, taasisi na viongozi waliofanya vizuri katika kipindi cha miaka 10, Tuzo hizo safari hii zimekuwa tofauti na miaka yote kwani waliopewa Tuzo ni wale waliofanya vizuri katika kipindi cha miaka kumi.
DSC_0065
Shadrack Nsajigwa akipokea Tuzo kwa niaba ya timu iliyofanya vizuri katika mashindano ya CHAN
Tuzo hizo ambazo zilikuwa maalumu mwaka huu, kwani zimetumika kumuaga RaisKikwete kwa kumaliza muda wake madarakani na kuheshimu mchango wake katika kuinua michezo nchini katika kipindi cha utawala wake. Ikumbukwe kuwa Tuzo hizo ziligawanyika katika vipengele vinne, Taasisi iliyochangia kuinua michezo katika kipindi cha miaka kumi Tuzo 5.
DSC_0075
Francis Cheka akipokea Tuzo yake
Tuzo zimetolewa kwa wanamichezo waliofanya vizuri katika kipindi cha miaka kumi, viongozi waliochangia kuinua michezo katika kipindi cha miaka kumi Tuzo 5 na Tuzo ya heshima kwa Mh Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuheshimu mchango wake katika kuinua michezo wakati wa utawala wake, baadhi ya waliopewa Tuzo usiku wa October 12 ni Francis ChekaMbwana SamattaIddi KipinguAbdallah Majura na Hashim Thabiti
DSC_0053
DSC_0066
DSC_0068
Mama yake Hashim Thabiti akichukua Tuzo kwa niaba ya Hashim
DSC_0069
DSC_0071
Charles Mkwasa akichukua Tuzo ya Twiga Stars kwa kufanya vizuri katika kipindi cha miaka 10.
DSC_0079
Wawakilishi wa Mbwana Samatta wakichukua Tuzo kwa niaba yake
DSC_0082
DSC_0084
Kanali Iddi Kipingu akipokea Tuzo yake ya heshima kwa kusaidia kuinua michezo kwa muda mrefu toka yupo shule ya Makongo
DSC_0089
Rais Kikwete akimkabidhi tuzo Dioniz Malinzi kwa kujenga Uwanja wa Gofu Misenyi mkoani Kagera
DSC_0092
Rais wa zamani wa TFF Leodger Tenga kapata Tuzo ya kiongozi bora katika kuinua michezo
DSC_0094
Abdallah Majura akikabidhiwa Tuzo ya heshima katika kuinua michezo sasa kafungua kituo cha Radio kinachojihusisha na michezo.
DSC_0097
Mzee Said akipokea Tuzo ya Taasisi iliyochangia kuinua michezo nchini Azam SSB
DSC_0113
Mwenyekiti wa TASWA Juma Pinto akimkabidhi Rais Kikwete Tuzo ya heshima akiwa pamoja na mkuu wa mkoa Dar Es Salaam Meki Sadiki, waziri wa michezo Dk Fenella Mukangara na Dioniz Malinzi.
DSC_0118
DSC_0123
Nahodha wa Taifa Stars Nadir Haroub akikabidhi jezi ya Taifa Stars kwa Rais Kikwete ikiwa imesainiwa na wachezaji wote.
DSC_0149
Baada ya ugawaji wa Tuzo Rais Kikwete alipata nafasi ya kuongea na waandishi wa habari na wageni waalikwa katika Tuzo hizo.
DSC_0163
DSC_0170
DSC_0187
Rais Kikwete katika picha ya pamoja na watu mbalimbali
DSC_0202
Rais Kikwete katika picha ya pamoja na washindi wa Tuzo hizo
DSC_0221
Yamoto Band wakaitimisha kwa kuwachezesha waandishi wa habari kimadoido

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...