Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, November 8, 2015

BONDIA IBRAHIMU TAMBA KUPAMBANA NA BARAKA MWAKANSOPE WA MBEYA NOVEMBA 22 MANZESE


Na Mwandishi Wetu 
BONDIA Ibrahimu Tamba anapanda tena uringoni Novemba 22 katika ukumbi wa Frends Corner Manzese Dar es salaam kugombania mkanda wa ubingwa na bondia Baraka Mwakansope  kutoka Mbeya  kg 73 mpambano uho wa raundi kumi

unatalajiwa kuwa wa kisasi baada ya mara ya kwanza Tamba kumsambalatisha bondia Maisha Samsoni wa uko uko Mbeya hivyo mwakansope amekuja kwa ajili ya kulipiza kisasi cha kupigwa kwa mwenzake mpambano uliofanyika mwanzoni mwa mwaka huu

mratibu wa mpambano uho Jaffar Ndame ameongeza kwa kusema kuwa siku hiyo kutakuwa na mapambano mawili ya ubingwa ambapo bondia Julius Kisalawe atapambana na Ramadhani Kumbele kg 51 ubingwa wa Taifa mpambano wa raundi kumi

mpambano mwingine utawakutanisha bondia Pius Kazaula wa Morogoro atakaepambana na Abdallah Luwanje wakati bondia chipkizi kutoka Super D Boxing Promotion Vicent Mbilinyi atakabiliana na Said Tampoo kutoka bagamoyo

aliongeza kuwa siku hiyo kutakuwa na mapambano mengine ya mabondia chipkizi  mbali mbali pia kutakuwa na burudani za kutosha hivyo kawaomba wapenzi na mashabiki wa mchezo wa masumbwi kuwai ukumbini kwa michezo itanza rasmi kuanzia saa 11 jioni na kumalizika mnamo saa tano kasoro usiku
Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi
pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Kocha Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...